LOWASSA AMSHINDA MAGUFULI TENA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Edward Lowassa, aliyekuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Ukawa, akiwasili kwenye ukumbi wa Karimjee |
EDWARD Ngoyai Lowassa, sasa anaongoza rasmi jiji la
Dar es Salaam. Ni baada ya Isaya Chares Mwita, aliyekuwa mgombea wa kiti cha
umeya, kutangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho, anaandika Saed Kubenea.
Isaya aligombea nafasi hiyo,
kupitia vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Lowassa,
waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri, alikuwa mmoja wa wagombea urais katika uchaguzi
mkuu uliyopita.
Pamoja
na kwamba hakutangazwa kushinda, lakini alitoa upinzani mkali na wengi
wanaamini kuwa ndiye aliyestahili kutangazwa mshindi.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo, uliofanyika katika ukumbi wa Karimejee, Jumanne 22
Machi 2016, Sarah Yohona, Kaimu Mkurugenzi wa jiji alisema, Isaya alipata kura
84 kati ya 151 zilizopigwa.
Kinyang’anyiro
cha uchaguzi wa umeya wa jiji kimefanyika miezi mitano baada ya kumalizika
uchaguzi mkuu.
Aidha,
uchaguzi wa meya wa jiji umefanyika baada ya mbinu kadhaa za chama tawala –
Chama Cha Mapinduzi – kuzuia uchaguzi huo kushindwa kufanya kazi.
“Kwa
matokeo haya, Lowassa ndiye aliyeibuka kidedea. Yeye ndiye atakayeongoza jiji
la Dar es Salaam. Magufuli (John Pombe Magufuli, rais wa Jamhuri) atakuwa chini
yake,” anasema Penina Nkya, mmoja wa viongozi wa Chadema.
Naye
Omari Thabiti Kombo, diwani wa Kata ya Makurumla (CUF) amesema, “ushindi
tulioupata siyo wetu. Ni wa Lowassa.”
Anasema,
“…tumetimiza kile ambacho tulikuwa tunakipigania kwa muda mrefu. Leo tumetoka
kifua mbele na hii ni zawadi kwa Lowassa ambaye alikuwa mgobea wetu urais.”

No comments
Post a Comment