Zinazobamba

WAZIRI NANAUKA AWATAKA VIJANA KUWA WAZALENDO.


*Awasihi kuheshimu Sheria,kulinda amani. .

Na Moses Mashala 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Joeli Nanauka amewataka vijana wa Tanzania kuwa wazalendo, wachapakazi wenye nidhamu. 

Waziri Nanauka ametoa rai hiyo leo Desemba 23,2025 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea utekelezaji wa mipango ya Wizara yake katika Serikali ya wamu sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Aidha amesema kuwa Vijana wanapaswa kuheshimu sheria,walinde amani na mshikamano wa Taifa,na wajitokeze kwa ujasiri kushiriki katika shughuli za maendeleo. 

"Kauli mbiu yetu ya "Vijana Tuyajenge, Tanzania ni Yetu" si maneno matupu,bali ni wito wa vitendo kwa kila kijana kutambua kuwa Taifa hili ni lao na wana wajibu wa kulilinda" amesema Nakuongeza kuwa "Nawahakikishia vijana wote wa Tanzania kuwa ofisi yangu iko wazi,katika kutoa huduma kwa vijana,tutazingatia falsafa yetu ya kutoa huduma kwa kasi,vituoni kufikika kwa urahisi,

na kutumia teknolojia,ikumbukwe kuwa jukumu kubwa la Wizara ni kuweka mazingira wezeshi kupitia sera,sheria, kanuni na miongozo pamoja na kuratibu shughuli za maendeleo ya vijana nchini."

No comments