SOKO LA HISA LAWATANGAZIA NEEMA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Meneja Masoko wa DSE Patrick Mususa wakati wa mkutano na waandishi wa Habari
NA KAROLI VINSENT
SOKO la hisa mkoani Dar es salaam (DSE) limewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kujitokeza kwa wingi katika shindano la (Schollar investment challenge) ili
kuweza kupata fursa mbalimbali za kibiashara
nakukuza uelewa juu ya utendaji kazi wa soko hilo kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo
jijini Dar es salaam Meneja Mauzo na Biashara wa DSE Partick Mususa amesema
katika kuhakikisha shindano hilo
linafanikiwa taasisi hiyo imeamua kuwateua mabalozi mbalimbali katika vyuo vishiriki katika shindano
hilo ikiwa ni sehemu yakukuza hamasa juu yashindano hilo
.
Mususa amesema Mabalozi watakaoteuliwa katika
shindano hilo ni mabalozi kutoka vyuo mbalimbali vikuu ambavyo ni pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM,Chuo
Kikuu cha SOKOINE, Chuo cha usimamizi wa fedha IFM, Chuo kikuu cha Dodoma UDOM ,Pamoja
na chuo cha Mipango miji Dodoma IRDP ,
Mususa ameeleza kuwa kupitia mabalozi wa vyuo hivyo
wanategemea kupata hamasa ya kushiriki
kwa wanafunzi katika shindano hilo .
Mususa ameongeza kuwa kupitia mabalozi watakao teuliwa
nasoko hilo la hisa la Dares salaam chuo ambacho kitakuwa na mabalozi wengi zaidi
ndicho kitapewa nafasi zaidi yakushinda nakuweza kupewa fursa mbalimbali zinazo
tolewa na soko hilo
.
Mususa amebainisha kuwa sambamba nakutoa hamasa kwa wanafunzi hao na kuweza kujiunga na shindano hilo aliviambia vyombo vya habari kuwa
mabalozi watakao chaguliwa
na taasisi hiyo wataweza kupata fursa za kuwekeza katika makapuni
mbalimbali yanayo uza hisa zake kupitia soko hilo.
"wanafunzi hawa wa vyuo vishiriki wa shindano letu
la scholar invest ment Challenge
watatapatafursa mbalimbali ikiwemo kununua hisa na kudhaminiwa na hata kupewa ajira baada ya kushiriki
katika shindano letu "Aliendelea kueleza Meneja huyo wa Mauzo na Biashara
No comments
Post a Comment