MAKONDA AANZA 'KUVIMBA KICHWA'ASEMA AMUOGOPI RAIS MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA

PAUL Makonda,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amedai kwamba hafanyi kazi kwa kumwogopi Rais
John Magufuli, anaandika Regina Mkonde.
“Nafanya kazi zangu ipasavyo na si kwa woga wa
rais. Namuomba Mungu anisaidie nisitumie cheo na madaraka yangu kugandamiza
wengine,” amesema Makonda.
Hata hivyo, Makonda amejidhihirisha kuwa kiongozi mbabe. Mwaka
juzi alimvamia Jaji Joseph Warioba, katika mdahalo wa katiba Mpya, jijini Dar
es Salaam, akamrushia makonde na mdahalo ukavunjika.
Baada ya hapo aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Desemba mwaka jana, alitumia mamlaka yake vibaya kwa kuamuru polisi wamkamate
Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo, baada ya wawili hao kutofautiana kauli wakiwa
kwenye usuluhishi wa mgogo wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Tooku na
menejimenti, jijini Dar es Salaam.
Makonda alitoa kauli hiyo jana wakati akikabidhiwa ofisi na Said
Mecky Sadick, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Sadick amehamishiwa
mkoani Kilimanjaro kushika wadhifa huo.
Kwenye makabidhiano hayo Makonda amevitaka vyama vya upinzani
kuachana na siasa za ubaguzi na kwamba, wanapaswa kufanya siasa wakati uchaguzi
utapokaribia.
“Huu si wakati wa kuendekeza siasa za kibaguzi, si wakati wa
propaganda za kuchafuana, tufanye kazi. Wananchi wanahitaji kuona mabadiliko
kama mlivyokuwa mnajinadi kwenye kampeni za uchaguzi, subiri mwanzoni mwa waka
2020 ndiyo muanze siasa.
“Nitafanya kazi kwa kuzingatia kanuni, katiba na ilani ya CCM
katika kutatua changamoto za Jiji la Dar es Salaam,” amesema Makonda.
Akikabidhi ofisi hiyo, Sadick alimwambia Makonda kwamba jiji
hilo haliongozwi na upinzani kama ambavyo inaelezwa na vyama hivyo.
“Dar es Salaam haijakamatwa na upinzani, bali ni mameya na
wabunge ndiyo wengi. Hii haimaanisha kwamba jiji linashikwa na upinzani,”
amesema Sadick.
Kwenye makabidhiano hayo Sadick amesema, atakapokwenda kuanza
kazi Mkoa wa Kilimanjaro hatapambana na vyama vya siasa bali atashughulikia
maendeleo.
“Siendi kupambana na vyama vya siasa mkoani Kilimanjaro,
ninakwenda kusimamia maendeleo, awe kiongozi wa CCM au Chadema sawa, sote tuna
nia ya kujenga nyumba moja,” amesema
No comments
Post a Comment