SAKATA LA WABUNGE WA CCM KULA RUSHWA.LACHUKUA SURA MPYA,WAZIRI WA MAGUFULI ASEMA YA MOYONI,SOMA HAPO KUJUA

Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea kuchunguza tuhuma
zinazowakabili baadhi ya wabunge kwa kupokea rushwa kwenye Kamati za Bunge,
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, amesema
Bunge linapaswa kujisafisha.
Mabula ambaye pia ni
Mbunge wa Ilemela, alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Nipashe baada ya
kumalizika kwa ibada ya mkesha wa Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro.
Alisema kama tuhuma za
rushwa zinazoelekezwa katika Bunge zina ukweli, Bunge linapaswa kujisafisha kwa
kuwa ni mojawapo wa mhimili wa serikali unaotumainiwa na wananchi.
Alisema Watanzania
wana imani kubwa na wabunge katika kuwatatulia kero zao kwa kuwa wao ndiyo
wawakilishi wa wananchi, hivyo tuhuma zinapowakabili wanapaswa kijisafisha na
kuwa wasafi.
“Siwezi kuzungumza kwa
undani zaidi kwa kuwa sote hatujui kama ni kweli au la, lakini ninachoweza
kusema ni kama tuhuma hizo zina ukweli, basi Bunge linapaswa kujisafisha,”
alisisitiza Mabula.
Kadhalika, amewaasa
Watanzania kutenda matendo mema wakati wote.
Kumekuwapo na tuhuma
za rushwa kwa baadhi ya wenyeviti wa Kamati za Bunge, huku wabunge wengine
wakijiuzulu kwa kutaka mamlaka za kiuchunguzi wachunguze tuhuma hizo na sheria
ichukue mkondo wake.
Baadhi ya wabunge
wanaotuhumiwa kupokea rushwa ni wa Kamati ya Maendeleo na Huduma za Jamii, hali
iliyosababisha wabunge 12 katika kamati hiyo kusaini waraka maalum wa kupelekwa
kwa Spika kutaka kujiuzulu, huku Spika wa Bunge, Job Ndugai, akifanya
mabadiliko ya wenyeviti watano wa kamati hizo.
CHANZO:
NIPASHE
No comments
Post a Comment