TUNDU LISSU NI KIBOKO AIBWAGA TENA CCM MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
MAHAKAMA Kuu
Kanda ya Dodoma leo imefutilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa
na mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jonathan Njau kupinga ushindi wa
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu (Chadema). Anaandika Dany Tobason, Dodoma …
(endelea).
Katika madai yake ya msingi, Njau alikuwa
akipinga matokeo na kutaka kura kuhesabiwa upya. Shauri hilo lilikuwa
mbele ya Jaji Berkel Sehel.
Njau alishindwa kwenye uchaguzi kwenye jimbo hilo mwaka 2010 na
2015. Njau aliwasilisha ombi mahakamani kwa kutaka kesi hiyo kufutwa
kwani hana haja ya kuendelea na shauri hilo.
Awali mlalamikaji aliwahi kupeleka mahakamani mara mbili maombi
ya ombi la kusamehewa kwa gharama za kesi kiasi cha milioni 15 lakini maombi
hayo yalitupwa na mahakama.
Akizungumza nje ya mahakama baada ya shauri hilo kutupwa Lissu
amesema aliweka hoja sita za kupinga uhalali wa kesi hiyo hata angelitoa Sh.
milioni 15 angeshindwa kwenye mapingamizi.
“Kesi aliyofungua mwaka 2010 ilikuwa na makosa yale yake hakuna
kilichobadilishwa labda jina, tarehe na mwaka,” amesema Lissu na kuongeza:
“Hii kesi ingekuka tu kwa sababu ililetwa bila umakini wowote
makosa mbalimbali ya kisheria yalikuwepo hata angelipa milioni 15 angeondolewa
tu kwenye pingamizi.
“Hakuna aliyobadilisha, wakati ule alifunguliwa kesi na wapambe
wake lakini baadae sheria ikabadilika.
“Narudia rai niliyotoa wiki mbili zilizopita kwenye kesi ya
pingamizi iliyofunguliwa na Injinia Christopher Chiza makosa yale yale hawa
watu wanafundishana.”
Lissu amesema Mahakama Kuu ilishatamka mwaka 2010 kuwa kesi za
uchaguzi si za kuendelea kwa papara bila umakini wowote, bila wakili kutekeleza
vitu rahisi rahisi vya kisheria.
“Sipunguziwi kasi mahakamani, kesi za uchaguzi nilianza kufanya
miaka 10 iliyopita mtu ambaye alishtakiwana CCM nilisimamia kesi hizo,” amesema
Lissu.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni