BARAZA LA MITIHANI LATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA NNE,SOMA HAPO KUJUA
BARAZA la Mitihani nchini (NECTA) limetangaza
matokeo ya darasa la nne huku wanafunzi 977,888 wamefaulu na kuendelea darasa
la tano na pia wanafunzi 108829 wamepata daraja la E ambao ufahulu wao ni hafifu
na kutakiwa kakalili darasa la nne tena.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na
waandishi wa habari,Katibu mtendaji mkuu wa (NECTA),Dkt Charles Msonde amesema
jumla ya wanafunzi 1,037,305 waliosajiliwa kufanya upimaji wa mtihani wa darasa
la nne mwaka 2015 wakiwemo wasichana
535,273 sawa na asilimia 51.60 na wavulana 502,032 sawa na asilimia 48.40,
Dkt ,Msonde amesema wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 94.27 ndio waliofanya mtihani
huo,ambapo wanasichana walikuwa 510,221 sawa na asilimia 93.16 na wavulana
walikuwa 467,675 sawa na asilimia 93.16 huku wasiofanya walikuwa ni 59,416,
Dkt,Msonde amezitaja changanuo za mtokeo hayo,ambapo
amesema inaonyesha kuwa jumla ya
wanafunzi 977,886 wamefanya vema kwa
kupata alama za A,B,C,D,na wanafunzi 108,829 sawa na asilimia 11.3wamepata
alama za daraja la E lenye ufahulu usioridhisha,
Hata hivyo,Dkt
Msonde amesema katika matokeo hayo wanafunzi wamefanya vema katika masomo ya
sayansi ambapo ufaulu wake umekuwa ni asilimia 89.44 na somo waliofaulu kwa
kiwango cha chini zaidi ni somo la English Language lenye ufaulu wa asilimia
65.67.
Vilevile Dkt Msonde amezitaja shule kumi bora
zilizofanya vizuri katika mtihani huo ni
Alliance mwanza,waja springs Geita,St Peter mkoani Kagera,Tumaini mkoani
Mwanza,Furaha Mkoani Mwanza,Acacia Land mkoani Tabora,Tusiime mkoani Dar es
Salaam,Imani mkoani Kilimanjaro,Kaizerege mkoani Kagera na Ebenezer mkoani
Kilimanjaro.
Pamoja na hayo,Dkt Msonde pia aliwataja wanafunzi kumi bora kitaifa waliongoza mtihani ambao ni Frank
Mgeta kutoka shule ya Twibhoki mkoani Mara,Salim Rashid kutoka shule ya Hazina
mkoani Dar es Salaam,Musa Christian kutoka shule ya Alliance mkoani Mwanza
,Ezekiel Gilu kutoka shule ya Waja Springs mkoani Geita,
Wengine ni Martha Nkwimba kutoka shule ya Tusiime
mkoani Dar es Salaam, Lameck Nsulwa kutoka shule ya Rocken Hill mkoani
Shinyanga,Rajabu Mhoja kutoka shule Rocken Hill mkoani Shinyanga,Charles
Luhumbika kutoka shule ya Kwema mkoani Shinyanga,Mathias Amos kutoka shule ya
Alliance kutoka mkoani Mwanza pamoja na Idd Masudi kutoka shuke ya Alliance
mkoani Mwanza.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni