Zinazobamba

WATAALAMU WA UBUNIFU MAJENGO NA UKADIRIAJI MAJENZI WATAKIWA KUWA WAZALENDO.

Na Mussa Augustine.

Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji  Majenzi wametakiwa kuwa wazalendo ili kuhakikisha wanatekeleza kwa wakati miradi ya ujenzi wanayopatiwa na Serikali au sekta binafsi.

Rai hiyo imetolewa leo Oktoba 29,2024 Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Edward Mpogolo ambaye alikua amemwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Mashaka Biteko wakati wa Mkutano wa  tano wa Bodi ya wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNICC)

DC Mpogolo amesema kuwa baadhi ya wataalamu wa ubunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi wamekua wakiangalia maisha yao binafsi kwa ajili ya kujipatia fedha kwa muda mfupi huku suala la weledi kazini likiwa limewekwa pembeni hali ambayo inasababisha majengo kuwa chini ya kiwango.

Amesema kwasasa serikali ipo kwenye mchakato wa kufanyia maboresho sera ya ujenzi ili kutengeneza Sheria ya ujenzi itakayosidia  wataalamu hao kufikia matamanio ya kukuza sekta ya ujenzi kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kwa kasi Duniani.

"Jitihada zinazopatikana katika sekta ya ujenzi inatokana na nyinyi wataalamu wa ubunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi,ukiona mafanikio yaliyopo kwa sasa yanatokana na nyinyi,hivyo kwa niaba ya serikali  nawaomba sana muwe Wazalendo ili tumuunge mkono Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan" amesema DC Mpogolo.

Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt.Daudi Kondoro ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania( TBA) amesema kuwa watendaji wa Wizara wataendelea kusimamisha sekta ya wataalamu wa ubunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi ili waweze kua na weledi katika kazi zao.

"Wizara ya ujenzi itatenga fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa mafunzo wataalamu 180 Kila Mwaka ambao wanahusika na bunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi,ili waweze kuwa na uelewa Moana katika taaluma yao" amesema Dkt.Kondoro.

Na Mwenyekiti wa Bodi ya usajiri  wa wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) Dkt Ludigija Bulamile amesema kuwa kwa sasa Bodi hiyo imesajili 1586 ambapo kati yao 33 ni wageni kutoka nje ya nchi.

Mkutano huo wa tano wa Bodi ya wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB) umeenda sambamba na mahafali ya kwanza ya wahitimu wa mafunzo ya taaluma ya wabunifu Majengo na wadiriaji Majenzi ,ambapo zaidi ya wahitimu 130 wamehitimu na kutunukiwa vyeti na mgeni rasmi.

Hakuna maoni