Zinazobamba

TFDA KANDA YA MASHARIKI WAFANYANYA UKAGUZI ELEKEZI SOKO LA ILALA, WAWATAKA MAMA LISHE BABA LISHE KUFUATA UTARATIBU WA USAFI...




Meneja wa mamlaka ya chakula na dawa Kanda ya Mashariki, Emanuel Alphonce akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza na wafanyabiashara wa chakula(baba lishe na mama lishe) katika soko la Ilala jijini Daresalaam. Emanuel alifika katika soko hilo na wafanyakazi wengine wa mamlaka hiyo kufanya ukaguzi elekezi kuhusu chakula Salama


Mmoja wa wafanya biashara wa chakula soko la Ilala akimuhudumia mteja wake chakula. TFDA walifika hapo kufanya ukaguzi elekezi, kuona kama utaratibu wa kuandaa chakula salama unafuatwa

Sehemu ya wateja waliokuwa wanakula chakula katika sehemu isiyo salama,katika ukaguzi huo ilibainika kuwa wananchi wanakula chakula katika mazingira hatarishi kutokana na eneo kujaa maji machafu. Akizungumzia suala hilo Makamu Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao amesema hali hiyo imesababishwa na kunyesha kwa mvua lakini siku zote wamekuwa wakifuata taratibu zote za kuandaa chakula salama kwa afya ya walaji.


Jengo wanalofanyia biashara ya chakula likiwa katika hali hiyo... wafanyabiashara hao walilalamika kuwa wanapata shida zaidi wakati wa mvua na hiyo ni kutokana na nyumba wanayofanyia kazi kuwa katika hali mbaya, inavuja na hakuna anayejali juu ya tatizo hilo licha ya kulalamika mara kwa mara
Maafisa  wakifanya ukaguzi elekezi katika soko la chakula Ilala, hapo ni ndani na wanajaribu kutafuta eneo la kupita...zinazoonekana ni meza zinazotumika kwa chakula...

Emanuel Alphonce akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu hali aliyoikuta katika soko hil, Meneja huyo amesema wanatambua kuwa nyakati za mvua hali huwa mbaya katika masoko mengi lakini wao wamepita kuangalia na kutoa elimu juu ya chakula salama...

Hakuna maoni