TAMONGSCO WAIPONGEZA SERIKALI KUFUTA MFUMO WA GPA NA KURUDIA WA DIVISION
Shirikisho
la wamiliki wa shule na vyuo visivyo vya serikali TAMONGSO watoa
pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na
Ufundi kwa kuliagiza Baraza la Taifa la Mitihani kufuta mfumo unaotumika
sasa wa Wastani wa Alama (GPA) na kurudi katika mfumo uliokuwa
unatumika hapo awali wa division.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Taifa wa
TAMONGSO Bwa. Mrinde Mzava amesema kuwa Waziri wa Elimu Ameitendea haki
Sekta ya Elimu kwani mfumo huo ulileta sintofahamu kwa wananchi wengi.
“Waziri
ameitendea haki sekta ya Elimu kwani mfumo wa GPA ulileta sintofahamu
kwa wananchi na pia ulikuwa unaongeza ufaulu usio na mashiko kwa
wanafunzi walio wengi ukilinganisha na mfumo uliokuwa unatumika awali,” aliongeza Mwenyekiti huyo.
Vilevile
Mwenyekiti huyo alisema kuwa Tanzania inahitaji kuingia kwenye soko la
upinzani hasa katika sekta ya Elimu ili iweze kuajiri watu wenye
utaalamu na sifa stahiki na kuweza kushindanishwa kwenye soko la
kimataifa hivyo kwa mfumo wa GPA ulikuwa unadidimiza elimu ya Tanzania.
Mbali
na hayo Mwenyekiti huyo alitoa agizo kwa baadhi wamiliki wa shule na
vyuo visivyo vya Serikali kutotumia kigezo cha pesa ili kudidimiza
kiwango cha Elimu nchini.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bwa. Emmanueli
Gwegenyeza ameshauri viongozi na wananchi kwa ujumla kutochanganya suala
la Siasa na Elimu kwani kwa kufanya hivyo tutazidi kudidimiza Sekta ya
Elimu nchini.
“Tusiingize
suala na Siasa na Elimu kwa wakati mmoja kwani kwa kufanya hivyo
tunaweza kuididimiza Sekta ya Elimu pia tunaahidi kumpa Waziri
ushirikiano ili kuzidi kuinua Sekta ya Elimu nchini,” aliongeza Makamu huyo.
Maoni 1
UAMUZI WA WAZIRI NDALICHAKO KWA NAMNA MWINGINE MI SI UPONGEZI KWANI,NI WA KISIASA ZAIDI.HII INAONYESHA JINSI TAIFA LETU LINAVYOPELEKWA VIBAYA NA VIONGOZI HATA MIE NINGEFANIKIWA KUWA WAZIRI NINGEWEKA MFUMO WANGU.SASA BASI HATA KAMA WATANGULIZI WAKE WALIKOSEA ANGETAFUTA NAMNA YA KUTATUA TATIZO HILI LIPATIWE UFUMBUZI WA KUDUMU SI VINGINEVYO.
Chapisha Maoni