DKT KIKWETE AWA MKUU WA CHUO MPYA WA CHUO KIKUU DARESALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(Chancellor of the University of Dar es salaam).
Rais Mstaafu Kikwete anachukua nafasi hiyo, iliyoachwa wazi na
Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliyefariki dunia Februari, 2014.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Ikulu
Jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 17
Januari, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni