WAZIRI NAPE AMTIA DOA MAGUFULI,JUKWAA LA WAHARIRI WAMCHAKAZA TENA,NI KUHUSU UBABE WAKE KULIFUNGIA GAZETI LA MAWIO,SOMA HAPO KUJUA
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania ( TEF), Nevelle Meena (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kushoto ni Mwenyekiti wa TEF,. Absalom Kibanda |
JUKWAA la
Wahariri Tanzania (TEF) limelaani hatua ya serikali kulifutia usajili gazeti la
MAWIO na kwamba ni ukandamizaji wa vyombo vya habari nchini. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Jukwaa
hilo limeeleza kwamba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye habainisha sababu za msingi za kulifuta gazeti hilo katika daftari la
Msajili wa Magezeti.
Kauli hiyo
imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu wa TEF, Nevelle Meena ambaye
amezungumza kwa niaba ya wahariri na kusema kuwa, sheria kandamizi zinatakiwa
kufutwa haraka iwezekanavyo kwani zinaminya uhuru wa vyombo vya habari.
“Tunajiuliza,
ikiwa ni miezi mitatu tu tangu Rais Magufuli aingie madarakani tayari amechukua
hatua ya kulifuta gazeti, itakuwaje katika safari yake ya miaka mitano? Sidhani
kama kuna chombo kitachopona,” anesema Meena.
Amesema mfumo uliopo
sasa wa kushughulikia matatizo au kasoro za kitaalama katika vyombo vya habari
ni kandamizi kwani unamfanya waziri kuwa ‘mhariri mkuu’ na amepewa mamlaka ya
kutoa adhabu kwa namna fikra zake zinavyomtuma hata fikra hizo zikikinzana na
misingi ya kaaluma.
Meena amesema
kwamba, wanapinga uamuzi wa kufutwa MAWIO kwasababu, TEF inaona uamuzi wa
serikali una nia mbaya kutokana na ukweli kwamba ufafanuzi wa kufutia usajili
wa gazeti hilo haikuwekwa wazi na wala haikufafanua lini wahariri wa gazeti
hilo walionywa.
Sababu nyingine
aliyoeleza Meena ni kuwa utaratibu uliotumika kufuta MAWIO ni ule ule wa
matumizi ya sheria kandamizi ya magezeti ya 1976 ambayo takribani kwa miaka 20
imekuwa ikipigiwa kelele kutokana na kumpa mtu mmoja (waziri) mamlaka ya kuamua
suala kubwa la kuwanyima watu haki ya kupata habari.
Meena amesema mfumo
wa aina hiyo ni kichaka ambacho serikali imekuwa ikitumia kufanya kile ambacho
kimeandikwa katika taarifa ya waziri kwamba Wahariri wa MAWIO walionywa mara
kadhaa. Walionywa na nani? Wapi? Na kwa sababu zipi?.
Katibu huyo amesema,
mwenendo wa aina hii wa kufuta magazeti siyo tu kwamba anaathiri dhana nzima ya
utawala bora, bali inaliweka Taifa katika hatari ya kutumbukia katika uovu,
hasa pale wenye dhamana watakapofanya wapendavyo kwa kuwa tu vyombo vya habari
vitakuwa vimezibwa midomo.
Mwenyekiti wa TEF,
Absalom Kibanda amewaambiwa waandishi wa habari kuwa, kitendo kilichofanywa na
serikali ni kutia uoga wahariri na waandishi ili wasiandike habari za ukweli
kuihusu serikali na kwamba, hakikubaliki.
“Tumepigwa tena
serikali ya awamu ya tatu ilitupiga, ya nne ikatupiga na hii ya tano inatipiga
tena na inalengo la kuiuwa tasnia ya habari. Na serikali inazidi kujipaka
matope mbele ya wananchi,” amesema Kibanda.
Aidha, ameeleza
masikitiko yake juu ya Waziri Nnauye kwa kuchukua hatua hiyo muda mfupi baada
ya kukutana na wahariri ambapo katika kikao hicho alichofanya na wahariri
alionesha kushirikiana nao.
“Bado tunachukua
hatua za kungea na wamiliki wa MAWIO pamoja na wahariri ili kutafakari na
kuchukua hatua zaidi ambapo tutatoa tamko letu,” amesema.
Habari
hii kwahisani ya mwanahalisi olini
Hakuna maoni
Chapisha Maoni