Zinazobamba

SERIKALI YAKUBALI KUKAUKIWA KIFEDHA,SOMA HAPO KUJUA

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa

SERIKALI imekiri kukaukiwa kwa hazina yake hivyo kusababisha ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza kukwama. Anaandika Moses Mseti … (endelea).
Katika upanuzi huo, serikalia ilihitajika kuchangia kiasi cha Sh. 85 Bilioni kati ya 105 zinazohitajika, madau mwingine kwenye upanuzi huo ni Benki ya Maendeleo Afrika (BADEA) na Mfuko wa Maendeleo wa Nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OFID) ambao tayari wametoa Sh. 20 Bilioni kama walivyoahidi.
Mhandisi wa Mradi huo, Mbila Mdemu amesema hayo kwenye kilichoandaliwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Professa Makame Mbarawa na wafanyakazi Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA).
Upanuzi wa kiwanja hicho unahusisha kazi mbalimbali ikiwamo ya urefushaji wa barabara ya kuruka ndege na kutua  kwa mita 500, ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege, ujenzi wa jengo la abiria na mizingo,hadi  kukamilika kutagharimu billioni 105.
kwenye kikao hicho Mdemu amesema kuwa BADEA na OFID tayari ziliishachangia kiasi cha Sh. 20 Bilioni 20 kama zilivyoahidi lakini serikali mpaka sasa haijatoa fedha yeyote na kusababisha mradi kukwama huku mkandarasi akiendelea kuidai serikali.
“Fedha ambazo zimekuwa zikitengwa katika bajeti ya serikali ni kidogo ukilinganishwa na mahitaji halisi ya mradi wenyewe, fedha zinazotengwa kwenye bajeti zimekuwa hazitolewi kama ilivyokusudiwa,” amesema Mdemu.
Amesema licha ya kukosekana kwa kiasi hicho cha fedha kutoka serikalini bado mkandarasi wa mradi huo, Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) anaidai serikali Sh. 17 bilioni.
Hata hivyo amesema kufuatia kukosekana kwa fedha za kumlipa mkandarasi huyo, amesitisha shughuli za ujenzi tangu Mei mwaka jana na kwamba licha ya kufanyika mazungumzo na hazina lakini hakuna kiasi kilichotolewa.
Prof. Mbarawa kwenye kikao hicho amedai sababu zinazochangia kiasi hicho cha fedha kushindwa kutolewa ni kutokana na ukusanyaji mdogo wa mapato unaokusanywa na TAA.
Amesema TAA nchi nzima imekuwa ikikusanya Sh. 5 bilioni kwa mwezi sawa na Sh. 60 Bilioni kwa mwaka na kwamba,  serikali tayari ilikuwa imewawekea lengo la ukusanyaji wa mapato, kiasi cha Sh. 7.5 bilioni kwa mwezi ambachi kinafikia Sh. 90 au 100 kwa mwaka.
“TAA nchi nzima mnapaswa kujipanga kuanzia sasa, kukusanya billion 90 ama 100 kwa mwaka na suala hilo tayari uongozi ulikuwa umelikubali na nyie ili kupata fedha hizo ni lazima mkusanye mapato makubwa,” amesema Mbarawa

Hakuna maoni