Zinazobamba

KAMANDA SIRRO AWAPA ELIMU WAKAZI WA BUNJU,SOMAHAPO KUJUA

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Simon Siro amezindua kituo cha polisi cha muda kilichojengwa kwa nguvu za wananchi katika kata ya Bunju baada ya kukithiri kwa matukio ya kihalifu katika eneo hilo.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Akizungumza na wananchi wa kata hiyo jana jijini Dar es salaam kamanda Siro alisema kata ya Bunju ndio kata inayoongoza kwa matukio ya kihalifu na na biashara za magendo katika kanda ya Dar es salaam.
"Huku  kuna majambazi, vibaka wauza gongo, kituo hiki ninaimani kitawakomesha watu hawa ambao wanahatarisha amani katika jamii.

Alisema hali hiyo inatokana na kituo cha polisi cha Kata hiyo kuchomwa na wananchi baada ya mwenzao kugongwa na gari.

Pia alisema ni wakati wa familia kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa iwapo kuna mwanafamilia anayejihusisha na vitendo kwani wahalifu wapo latika familia na wanandugu wanatambua hilo.
 

Kuhusu kituo cha kudumu katika eneo hilo kamanda alisema,apelekewe ramani ili jeshi liweze kusaidia gharama za ujenzi.
 

Kwa upande wake mkuu wa polisi wilaya ya Kawe John Malulu ,alisema  huduma za kipolisi ni jambo linalotakiwa kupewa kipaumbele kwani jamii haiwezi kuwa salama.
"Hatuwezi kuishi bila huduma ya kituo cha polisi kwahiyo mbinu za kujenga kituo cha kudumu zifanyike haraka ili huduma za kipolisi ziweze kutolewa kwa wananchi"


Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Christopher Mfaume, alisema kitendo cha kutokuwepo kwa kituo eneo hilo ni chanzo cha uhalufu hivyo wamejipanga kikamilifu na kuwataka viongozi wa Serikali ya mtaa kujenga vikundi shirikishi ilikuweza kuweka ulinzi.

''Vijana hao tutawapa mafunzo kikamilifu ikikuweza kusaidia changamoto hii iliyopo ili isiendelee kuwepo katika eneo hili, na huu ni wakati muafaka wa kujenga mbinu ya kuwanasa waalifu hao'' alisema.
Nao wananchi wakizungumza kwa nyakati tofauti  mariamu  Ally na wenzake walisema kujengwa kwa kituo cha polisi sio suluhisho kwani askari wa kata ya Bunju wanafanya kazi kwa mazoea.
 

Tinataka askari wapya waje hawa waliopo wanatunyanyasa unatoa taarifa za uhalifu mwenye kosa anaachwa anakamatwa mtu mwema hatuwataki hawa tumewachoka"alisema

Hakuna maoni