RAIS MAGUFULI ALIVYPOKELEWA ARUSHA...AFUNGA MAONESHO YA YA ONESHA UWEZO MEDAN YA CHUO CHA KIJESHI MONDULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa
Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha waliojitokeza kumsalimia wakati
akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo Medani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma bango mara baada ya
kukabidhiwa na mwananchi mmoja katika eneo la Kona ya Nairobi Mkoani
Arusha
Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa
Arusha katika eneo karibu na chuo cha Arusha Tech. Wananchi hao
walifunga barabara ili wapate nafasi ya kumuona Mheshimiwa Rais Dkt.
Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mianzini Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati waufungaji
wa zoezi la Onesha Uwezo Medani lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji
la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati akielekea
kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo Medan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya
Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la Ufungaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenye uwanja wa
maonesho akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis
Mwamunyange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya
pamoja na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara baada ya kufunga zoezi
la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akishuhudia
matukio ya zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipewa maelezo ya zana
mojawapo ya Kivita katika Zoezi la Onesha Uwezo Medani Mkoani Arusha.
Picha na IKULU
…………………………………………………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunga “Zoezi la Onesha Uwezo
Medani” lililoandaliwa na kutekelezwa na Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
ambalo ni sehemu ya Jeshi la wananchi Tanzania katika eneo la
Lang’arurusu nje kidogo ya Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani
Arusha.
Akizungumza na Askari na Maafisa
wa Jeshi la wananchi Tanzania kabla ya kufunga zoezi hilo, Rais Magufuli
amesema katika awamu yake ya tano ya uongozi amedhamiria kulitumia
Jeshi la wananchi Tanzania katika kujenga uchumi, ikiwemo kuanzisha
viwanda na kampuni za ujenzi ili kuharakisha maendeleo.
Ametoa mfano wa kiwanda cha
Nyumbu ambacho kipo chini ya jeshi la wananchi Tanzania na kueleza kuwa
wakati umefika wa kukiimarisha na kukiendeleza kiwanda hicho, ili kiweze
kufanya uzalishaji mkubwa kwa manufaa ya nchi ikilinganishwa na hali
ilivyo hivi sasa.
“Zipo nchi nyingi ambazo
majeshi yao yanatumika katika uchumi na yanafanya kazi nzuri ya kupigiwa
mfano, wakati umefika na sisi kufanya hivyo. Hata hizi sare za jeshi na
viatu, hatuna sababu ya kuvinunua kutoka nje ya nchi, tunaweza
kutengeneza sisi wenyewe” Alisisitiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli amelipongeza Jeshi
la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuandaa “Zoezi Onesha Uwezo Medani”
ambalo limethibitisha uwezo, weledi na utayari lilionao katika jukumu
lake la kiulinzi.
Ameahidi kuwa ataendeleza juhudi
zilizofanywa na viongozi wenzake waliotangulia za kuliimarisha kwa
vitendea kazi na maslai ya wanajeshi ili liweze kutekeleza wajibu wake
bila vikwazo.
Pamoja na kuwapongeza Askari na
maafisa wa Jeshi la wananchi Tanzania walioshiriki katika zoezi hilo,
Rais Magufuli ameagiza Askari Mgambo na Askari wa Jeshi la kujenga Taifa
(JKT) walioshiriki zoezi hilo kuajiriwa na jeshi la wananchi Tanzania.
Akitoa maelezo ya awali kabla ya
hotuba ya Rais Magufuli, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.
Hussein Ali Mwinyi, amesema Wizara yake itaongeza na kusimamia juhudi
za kuliboresha jeshi hilo kwa zana, vifaa na maslai kwa wanajeshi ili
kuwajengea uwezo na morali ya kutekeleza majukumu yao ya kuilinda nchi,
pamoja na kutoa msaada stahiki kwa nchi zenye kuhitaji ulinzi wa amani
popote duniani.
Kwa upande wake Mkuu wa majeshi
ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Adolf Mwamunyange amemhakikishia Rais
Magufuli kuwa Jeshi la wananchi Tanzania lipo imara na litaendelea
kutekeleza majukumu yake kwa weledi, nidhamu ya hali ya juu na uzalendo
mkubwa.
Kabla ya kuwahutubia maafisa wa
jeshi la wananchi, Askari na wananchi waliohudhuria ufungaji wa “Zoezi
Onesha Uwezo Medani”, Rais Magufuli ameoneshwa zana mbalimbali za kivita
ikiwa ni pamoja na kushuhudia upigaji wa mizinga ya masafa mafupi,
masafa ya kati na masafa marefu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha
22 Januari, 2016
Hakuna maoni
Chapisha Maoni