GULAMALI ATEULIWA KUWA MJUMBE WA KAMATI YA PAAC...MWENYEWE AAPA KUTANGULIZA UTAIFA KWANZA
Mbunge Gulamali akiwajibika pamoja na wapiga kura wake, Gulamali kwa muda mchache aliokaa madarakani amekuwa ni kipenzi cha wengi jimboni Manonga. |
Mbunge huyo ameandika katika Ukurasa wake wa Facebook "Nakushukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kuchagulia kuwa Mjumbe wa Kamati
ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).Sasa nimepata nafasi ingine ambayo
nitaweza kulisaidia Taifa langu kwani ninaamini juu ya Uwajibikaji
zaidi, kwa wale waliozoea kufanya kazi kwa Mazoea wakae mkao wa
Kutumbuliwa tu hakuna namna ingine ya kuwasaidia." baada ya kufanikiwa kupata nafasi hiyo.
JITIHADA ZA GULAMALI JIMBONI MANONGA
Gulamali
ameziba bwawa la Maguliati katika kata ya Ziba na kutengeneza mitaro ya
maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa zao la mpunga
linalotegemewa na wakazi zaidi ya 600 katika kata ya Choma, pamoja na
kushiriki ujenzi wa choo katika shule ya msingi Njia Panda kata ya
Nkinga.
Mbunge huyo aliyeshinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kwa kura
31,485 sawa na asilimia 67.65% alianza kwa kuwashukuru wananchi wake kwa
kuzunguka katika kata zote 19 na kuanzisha ligi ya mpira katika vijiji
68 na kutoa jezi pamoja na mipira kwa kila kijiji.
Aidha Gulamali amewaomba wananchi wake kuonesha ushirikiano wa hali
ya juu ili aweze kutekeleza vyema kazi waliyomtuma ya uwakilishi na
watarajie mabadiliko na maendeleo makubwa katika jimbo lao.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni