UCHAGUZI WA ZANZIBAR SASA KURUDIWA 20 MARCH 2016, JECHA ATANGAZA RASMI
Tume
ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi
visiwani humo baada ya matokeo ya uchaguzi uliopita kufutwa.
Uchaguzi huo sasa utafanyika Jumapili tarehe 20 Machi.
Tangazo hilo limetolewa na mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha.
Jecha amesema tarehe hiyo iliamuliwa na tume baada ya mkutano hapo jana.
"Uchaguzi
huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na
Madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya
kampeni," amesema Bw Jecha.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni