UBOVU WA MABEHEWA YAWATESA WANANCHI,SASA WASOTEA NJIANI,SOMA HAPO KUJUA
Abiria wa treni ya reli ya kati wakisubiri treni yao iendengamae ili waendelee na safari ya Kigoma
ABIRIA zaidi ya
1000 waliyokuwa wakisafiri na treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), jana
wamekwama mkoani Dodoma na kushindwa kuendelea na safari kutokana kuanguka
treni ya mizigo kati ya Kituo cha Itigi na Kitakaa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Tukio la kukwama abiria hao limetokea jana saa
2:00 asubuhi mjini hapa mara baada treni hiyo ya abiria ilivyo kuwa ikitokea
Dar es Salaam kuelekea Tabora, Kigoma na Mwanza kuzuiwa na Mkuu wa Kituo cha
Dodoma.
Akizungumza na wandishi wa habari mjini hapa Mkuu wa Kituo hicho
cha Dodoma, Suzo Kazimoto, amesema uongozi wa TRL umemalizika kuzuia kuendelea
kwa safari ya abiria hao kutokana kuelezwa mapema kuwa huko waliko kuwa
wakielekea kumetokea ajali.
Amesema baada ya kupata taarifa ya kuanguka treni hiyo wameona
ni vema kuzuia katika kituo hicho kwa vile abiria hao wangeweza kupata huduma
zote za kijamii zinazohitajika baadala ya kuiruhusu kwani huenda wangeenda
kwamba katika eneo ambalo halina huduma hizo muhimu.
“Taarifa tulizonazo ni kwamba mafundi wako kwenye eneo
wanaendelea na kazi ya kurejesha na tumewatangazia abiria wetu kuwa safari yao
itaendelea kuanzia saa 12:00 jioni leo,” amesema Kazimoto.
Akizungumzia malalamiko ya abiria kwamba baadhi yao walikuwa
hawana fedha za kujikimu, Kazimoto, amesema wakati huo walikuwa wakikusanya
idadi halali ya abiria wenye tiketi ili aweze kufanya mawasiliano na Makao
Makuu Dar es Salaam kwa ajili ya kupata kibali cha kuwapatia abiria hao fedha
ya kujikimu.
“Hata kama leo, ni nusu siku kwamba benki zinafungwa mapema hilo
siyo tatizo tutaangalia kilichopo ili tuweze kuwa saidia abiria wetu,” amesema
Kazimoto.
Awali baadhi ya abiria walilalamikia uongozi wa Shirika hilo
kushindwa kujenga njia mbili tangu walipokabidhiwa reli hiyo na mkoloni kwani
kama kungekuwa na njia mbili kama ilivyo katika nchi nyingine safari yao
ingeendelea bila mvutano kama huo.
mmoja wa abiria hao, Khadija Salum ambaye alikuwa akielekea
Kigoma huku akiwa na mtoto mdogo alikuwa akilia njaa baada ya kuibiwa Sh.
70,000 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kujikimu wakati wa safari hiyo.
Pia, amesema kuwa baada ya kukwama katika kituo hicho baadhi ya
wafanya biashara walipandisha bei za bidhaa ghafla hivyo kuwaongezea ugumu
katika kumudu kununua bidhaa hizo ikiwemo maji ya kunywa na chakula.
habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni