TUKIO KUBWA JIJINI DAR LEO,LHRC YAAZIMISHA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU,JAJI MJULIA ATOA NENO,SOMA HAPO KUJUA
Bendi ya Jeshi la Polisi nchini nalo alikuwa nyuma kwenye maandamano ya kuazimisha siku ya Haki za Binadamanu nchiniyaliyofanyika kwenye Viwanja vya makumbusho jijini dar es Salaam, |
Wanafunzi Mbali mbali nchini Wakiwe kwenye Maandamano ya kuazimisha siku ya Haki za Binadamu nchini, Tukio hili ambalo limeaandaliwa na kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini,(LHRC) |
Wito umetolewa kwa watanzania pamoja na Serikali kuruhusu lugha za asili kutumika kujieleza na kujitetea katika sehemu mbalimbali ikiwemo mahakamani.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Akizungmza
katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu iliyoandaliwa na kituo cha
sheria LHRC iliyofanyika katika uwanja wa makumbusho ya Taifa leo Jijini Dar es
Salaam, jaji wa mahakama kuu,Aloyce Mjulia amesema kuwa watu wengi wanahukumiwa
kwa kushindwa kujieleza.
Amesema endapo mtu atapewa frusa ya
kutumia lugha anayiifahamu kwa kina ataweza kujieleza na kupata haki ya msingi.
“Mimi nina uzoefu kwa kazi hizi mara
nyingi hata askari wetu hawafuati masharti ya haki za binadamu kwani
wanapowakata watuhumiwa wanahoji maswali ambayo wanajua kwamba watajibiwa
wanavyopenda wao.,
“vile vile
mahakamani mtu anatakiwa kujitetea kwa kutumia lugha ambayo anaijua kwa kina na
awepo mtu wa kutafsiri lakini mara nyingi utakuta hii inatokea pale tu anapokuwepo
raia wa bkigeni,”amesema Jaji Mjulia.
Mgeni Rasmi wa siku ya Haki za Binadamu nchini Jaji wa Mahakama kuu nchini Aloyce Mjulia akimkabidhi cheti cha Pongezi Mwangalizi wa uchaguzi kwa kazi nzuri aliyofanya |
Kwa upande
wake Mwanasheria kutoka LHRC Bwana Sungusia amesema vitendo vya uvunjifu wa Haki
za binadamu nchini vimeongezeka sana huku akitolea mfano kipindi
kilichomalizika cha uchaguzi mkuu kwa kusema vyombo vya dola hususani polisi
wamekuwa ni watu wakutekeleza vitendo vya kinyama kwa raia.
“Vitendo vya
uvunjifu wa haki za binadamu vimeongezeka sana hapa nchini tumeshuhudia hata
kipindi cha uchaguzi,maana hata sisi haki za binadamu tumekuwa waathirika wa
kubwa,vifaa vyetu vy uangalizi mpaka leo vipo polisi,”amesem Sungusia.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni