WAFANYABIASHARA WAMPUUZA MAGUFULI,NI AGIZO LAKE LA SIKU SABA,KOVA ATANGAZA ZAWADI NONO ATAKAYEMDAKA HUYU,SOMA HAPO KUJUA
Kamanda wa Kanda Maalum Dar es
Salaam, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya
REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa
Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari
kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni
mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING
AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. Ameonyesha
picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo.
|
Makampuni 26 yamekaidi agizo la Rais John Magufuli
alilowataka wafanyabiashara wote waliokwepa kodi kwenye Makontena 326
yaliobainika kupotea bandarini walipe kodi ndani siku saba.Anaandika KAROLI
VINSENT endelea nayo.
Hata hivyo ni Makampuni 6 ndio waliolitii agizo la magufuli
baada ya kulipa kodi iliyokadiliwa
pamoja na Faini ambazo ni Bilioni 10.
Vilevile Makampuni 16 yamelipa kodi nusu tu tofauti na ile iliyokadiliwa,ambapo
siku ya leo ndio siku ya mwisho toka siku aliyosema Rais Magufuli kuwa ndani ya siku saba wawe
wamelipa kodi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mchana kwenye
Makao ya jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Meneja wa Huduma na
elimu kwa mlipa kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla
huku akiambata na Kamishna wa Kanda Maalum ya Polisi Suleiman Kova ,
Amesema mpaka
leo saa kumi jioni ni makampuni sita tu ndio yaliyolipa kodi hiyo huku mengine
16 yakilipa nusu ya madai ya kodi,huku Makampuni 26 yakishindwa kulipa kodi
iliyotakiwa pamoja na Faini ya kukwepa kodi.
“Agizo la Rais magufuli ndio mwisho wake leo saa
kumi jioni,lakini wafanyabiashara wenye Makampuni wamekaidi agizo hilo,kwahiyo
kama TRA hatuna chengine cha kufanya hapo tunaiachia mamlaka ya sheria kuchukua
hatua zaidi”amesema Bi Massala.
Bi Masalla ametaja makadilio ya kodi ambayo TRA ilifanya kwenye Makontena 326
yaliogunduliwa na Waziri mkuu wiki iliyopita pale alipofanya ziara ya
kushtukiza kwenye Bandari ya Dar es Salaam ni Bilioni 28 ambazo zilikuwa
zimepotea baada ya wafanyabiashara hao walikuwa wanataka kukwepa kodi.
Kwa Upande wa Kamisha Kova amewaambia wanahabari
kuwa Jeshi la Polisi linamtafuta Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI,
Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena
329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi .
Kamishna Kova amedai kuwa anayetafutwa na jeshi hilo
pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL
CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo.
Amesema Mwananchi atakayefanikisha kukamatwa kwa mtu
huyo (pichani) zawadi nono ya milioni 20 itatolewa kwa atakayefanikisha kutiwa
nguvuni.
Hata hivyo,Jeshi hilo pia linawashikilia watuhumiwa
40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi
unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato
Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489
yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.
Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)na
watumishi 03 kutoka Bandari kavu (ICD) YA AZAM wanatuhumiwa kuhusika na upotevu
wa makontena 329. Aidha, watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA) kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.
Kamisha Kova amesma uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za
forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika
mchakato huo. Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM
kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati makontena 2489
yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014
kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru.
Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini wote wanaohusika na hatimaye majalada ya
kesi yatapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika
kuhusika na makosa mbalimbali wafikishwe mahakamani
Hakuna maoni
Chapisha Maoni