MAGUFULI AANZA KUPATA DOA SASA,UTOAJI VYEO KWA WATUHUMIWA KWA UFISADI SOMA HAPO KUJUA
RAIS wa Tanzania, John Magufuli, amedaiwa kuanza
uongozi wa nchi kwa `kuhonga` wapambe na vigogo wa Serikali wanaotuhumiwa na
kashfa mbalimbali za ubadhirifu wa mali za umma katika kila kona. Anaandika Moses Mseti, Mwanza …
(endelea).
Rais Magufuli ambaye aliapishwa
Novemba 5 mwaka huu, kwa sasa ametimiza mwezi mmoja na siku nne tangu
achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uongozi
wa Rais Magufuli unatuhumiwa kuanza vibaya baada ya kuibuka madai ya
`kumhonga` nafasi ya Ukurugenzi kigogo anaetuhumiwa na kashfa kibao za
ubadhirifu wa mali za umma.
Uongozi
wa Magufuli umeanza kwa `kumhonga` nafasi ya ukurugenzi aliyekuwa Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Tito Mahinya, kuwa mkurugenzi wa Wilaya ya
Mbarali mkoani Mbeya.
Mahinya
ambaye ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa Mbarali, katika uchaguzi wa Oktoba 25
mwaka huu, aliahidiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwamba endapo atamtangaza
Mbunge wa sasa wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, angepata ukurugenzi jambo ambalo
limedhihilishwa.
Pia
Mahinya ambaye anatuhumiwa na kuwa ni `fisadi` wa kupindukia hivi karibuni
alipandishwa kizimbani baada ya kudaiwa kuuza viwanja vya wananchi wa
Nyamongoro Wilaya ya Nyamagana mkoani hapa vya Shilingi 60 millioni.
Pia
Mahinya anatuhumiwa ubadhirifu wa mabilioni ya fedha katika Jiji la Mwanza, ni
kati ya vigogo wachache katika Jiji hilo la wanaomiliki majumba ya kifahari,
shule na hoteli kubwa ambayo moja inadaiwa kuwa kona ya Bwiru (jina
linahidhiwa).
Hata
hivyo, inadaiwa kuwa baada ya Mahinya kumtanganza mbunge huyo wa Nyamagana,
kesi iliyokuwa ikimbabili katika Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, ilitupiliwa mbali
huku wananchi waliotapeliwa viwanja vyao wakiendelea kusaga maji.
Pia
inaelezwa kuwa Serikali ya CCM imeamua kumteua Mahinya na kumpeleka Mbalali mkoani
Mbeya kwa lengo la kumpa fadhila baada `kumchinja` aliyekuwa mgombea wa
Chadema, Ezekia Wenje, ambaye alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda.
Mahinya
ambaye kabla ya kuchaguliwa kuwa mkurugenzi wilayani Mbalali, alikuwa Afisa
ugavi wa Jiji la Mwanza, akitokea huko mkoani Mbeya ambaye hata huko inadaiwa
aliondolewa baada kuibuka kwa kashfa ya ubadhirifu wa fedha.
Mkurugenzi
huyo ambaye pia anatuhumiwa kuwa kinara wa kuandaa mipango na mikakati ya
`kuibia` Serikali, mwaka jana katika ubadhilifu wa billioni 40 katika
Halmashauli ya Jiji la Mwanza, kitendo chake cha ugavi ndo kilitajwa na PAC
kuongoza kwa ubadhilifu.
Hata
hivyo inadaiwa kuwa kitendo cha Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
kumteua Mahinya kuwa Mkurugenzi, imeelezwa ni mwanzo mbaya wa uongozi wa Rais
Magufuli ambaye ameanza kuongoza kwa `mbwembwe` nafasi hiyo.
Wasomi
na wataalamu wa masuala ya kisiasa waliozungumza na gazeti hili, wanadaiwa kuwa
kitendo cha uongozi wa Serikali ya Rais Magufuli kuanza kwa kuhonga vigogo
wanaotuhumiwa na ubadhilifu wa mali za umma, hautakuwa na tofauti na mtangulizi
wake, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete.
Wasomi
hao wanadaiwa kuwa ili uongozi wa Magufuli uwe tofauti na watangulizi wake
inapaswa asiteuwe vigogo wanaotuhumiwa na wizi wa mali za umma ama wenye chembe
chembe za wizi ili kujenga uchumi wa Taifa ulio imara.
Kijana
msomi na Mtaalamu wa siasa, John Nyanda, yeye alidai kuwa Rais Magufuli ambaye
ameanza kuongoza nchi kwa `mbwembwe` uongozi wake hautakuwa na utofauti wowote
kutokana na watu waliomzunguka kuwa ni vinara wa wizi.
Nyanda
alidai kuwa uteuzi wa Mahinya ambaye anatuhumiwa na kashfa kibao za wizi,
umeonesha ni namna gani Rais Magufuli, alivyoshindwa kuthibiti mianya ya uteuzi
mbovu uliofanywa na TAMISEMI kumteua mkurugenzi huyo.
“…,
aah uteuzi wa Mahinya uliofanywa na Tamisemi mimi nadhani ni fadhila tu, kwani
mtu kama huyo ambaye anatuhumiwa kwa kila kashfa katika Jiji la Mwanza lakini
leo hii anateuliwa kuwa mkurugenzi (Mbarali) hiyo ni dalii mbaya kwa uongozi wa
Rais (John Magufuli),” amesema Nyanda.
Mahinya
aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya baada wabunge wa
Tanzania kuapishwa Novemba 12 mwaka huu, Makao Makuu ya Tanzania mjini Dodoma,
ikiwa ni siku chache ya kuapishwa kwao.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni