Zinazobamba

DALALI WA ESCROW AULA UWAZIRI KWENYE SERIKALI YA MAGUFULI,YUMO PIA MWAKYEMBE WA MABEHEWA FEKI,SOMA HAPO KUJUA

Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akisalimiana na Waziri mku, Majaliwa Kassim.
Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akisalimiana na Waziri mku, Majaliwa Kassim

NA KAROLI VINSENT
PROFESA Sospeter Muhongo ambaye alitajwa kuwa ni Dalali  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakati ilipokuwa  inachunguzaufisadi wa sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),  sasa ameteuliwa kwa Mlango wa nyuma kuwa Waziri wa nishari na Madini.

Udalali wa Profesa Muhongo unatajwa kuwa ni pale alipotumia ofisi za umma kuwapatanisha Anayeejiita na Kuitwa mmiliki kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) Habirnder Seth Singh na Mmiliki wa kampuni ya Engineering and Marketing Limited (VIP)  bwana Rugemelira baada ya kutaka kutapeliwa Hisa zake na PAP.

Tuhuma hizo za udalali ndizo ndizo zikalifanya iliokuwa Bunge la 10 kuja maazimio ya pamoja ya kumtaka Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kumwondosha waziri huyo madarakani kutokana na kuhusika kwake huko jambo lilitekelezwa na Rais Kikwete kwa kumfukuza kazi Profesa Muhongo ambaye sasa amerejea tena wizara hiyo.
Profesa Muhongo amekuwa kiwatusi wawekezaji wa ndani kwa kusema hawana uwezo kuwekeza kwenye Gesi akidai hawana pesa hizo huku akisema "wanaweza kuwekeza kwenye juisi na machungwa tu"

Mbali na Profesa Muhongo,uteuzi mwengine aliofanya Magufuli leo ambao pia umeleta mashaka ni  wa Dkt Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Mwakyembe ambaye kwa sasa ameingia kwenye tuhuma lukuki za ufisadi ikiwemo ya kuhusika kwake au kunyamazia mpaka  kuitia hasara serikali ya Bilioni 230 kwenye ununuzi wa Mabehewa ya kubebea mizigo yanayotajwa kuwa ni feki,

Hata hivyo Mwakyembe huyu aliopewa ulaji huo, anatuhumiwa pia kuhusika au kunyamazia kwenye ufisadi wa kutupwa unaofanywa ndani ya Bandari ya Dar es Salaam mpaka kupelekea kupotea kwa zaidi ya Kontena 2000 kipindi yupo bado Waziri wa Uchukuzi kabla ya kuhamishwa kwenda wizara ya Afrika Mashariki.

Rais Magufuli amewatea mawaziri wengine ni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameendelea kuwa William Lukuvi ambapo Angelina Mabula ametajwa kuwa naibu wake. Wizara ya Maliasili na Utalii haijatangazwa waziri wake ambapo naibu waziri ametajwa kuwa ni Injinia Ramo Makani.

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji itaongozwa na Dk. Charles Mwijage lakini naibu waziri bado hajatangazwa. Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi bado hajatangazwa lakini nafasi ya naibu waziri imekwenda kwa Injinia Stella Manyanya.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto itaongozwa na Ummy Mwalimu ambapo naibu waziri wake ni Dk. Hamis Kigwangala.
Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo itaongozwa na Nape Nnauye ambapo Anastanzia Wambura akiwa naibu wake huku Wizara ya Maji na Umwagiliaji ikiwa chini ya Prof. Makame Mbarawa huku naibu wake akiwa Isack Kamwela.
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa ikienda kwa Dk. Augustine Mahiga ambapo naibu waziri akiwa Dk. Susan Kolimba.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa itaongozwa na Dk. Hussein Mwinyi ambapo naibu wake hajatangazwa. Wizara ya Mambo ya Ndani imekwenda kwa Dk. Charles Kitwanga ambapo naibu waziri hajatangazwa.


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora ina mawaziri wawili ambao ni George Simbachawene na Angela Kairuki, naibu ni Jafo Suleiman Said.
January Makamba ametajwa kuongoza Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira naibu wake akiwa Lugaha Mpina. Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira Vijana na Walemavu itaongozwa na Jenista Mhagama huku akisaidiwa na manaibu wawili ambao ni Dk. Abdallah Posi na Antony Mavunde.
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi itaongozwa na Mwiguli Nchemba huku William Tate Ole Nasha akiwa naibu waziri. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano haijatangazwa waziri wake ambapo naibu waziri ni Injinia Edwin Mgonyani.

Rais Magufuli hajatangaza waziri kwenye Wizara ya Fedha na Mipango lakini naibu waziri amemtaja kuwa Dk. Ashantu Kuaji. Wizara ya Nishati na Madini amekabidhiwa Prof. Mwijarubi Muhongo ambapo naibu waziri wake ni Dk. Mudadi Kaleman.

Hakuna maoni