MAWAZIRI WA MAGUFULI WAANZA KAZI NA MIKWARA,NAPE ANG'AKA KUFUNGIA MAGAZETI,MBARAWA,LUKUVI,JAFFO WALALAMA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Habari,utamaduni,Wasanii na Michezo,Nape Nnauye akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo,mara baada kuonyeshwa ofisi yake |
NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Wasanii
na Michezo,Nape Nnauye amewatohu hofu wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini
hususani Magazeti pamoja na wanahabari kwa kusema wanaozani kuwa kuchaguliwa
kwake na Rais John Magufuli kwenye wizara hio ni kwa ajili ya kuyafungia
magazeti,
Bali
amesema hata yafungia magazeti badala yake atahakikisha anakuwa mlezi wa vyombo vya habari pamoja waandishi wa
habari ili viweze kufanya kazi kwa weredi.
Akizungumza
na wafanyakazi wa wizara ya Habari na utamaduni,wasanii na Michezo wakati
alipokuwa akipokelewa na wafanyakazi wa wizara hiyo kwa mara ya kwanza tangu
achaguliwe kwenye nafasi hiyo na Rais Magufuli ambapo Nape amesema baada ya
Rais Magufuli kumchagua kuwa Waziri wa wizara hiyo waliibuka kundi la watu
wakisema magazeti yatafungiwa.
“Nawaomba
watu wa sekta ya habari kuondoa dhana ya kwamba mimi nitakuwa mtu wa kuyafungia
magazeti,kitu kama hicho akipo kwani nimekuja kwenye wizara hii ili wanahabri
wafanye kazi kwa weredi huku mimi nawahahidi nitakuwa mlezi wa vyombo vya habari”amesema
Nnauye.
Amesema nafahamu
kwa sasa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 imekuwa ikilalamikiwa sana ila kwa
upande wake amedai kuwepo kwa sheria hizo kwa wanahabari kunazidi wavunja moyo
wanahabari jambo analilohaidi kulishughulikia
.
.
Hata
hivyo Nape ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mtama,amewaomba wanahabari pamoja na
wamiliki kuhakikisha wanafanya kazi kwa weredi ili kuhakikisha wanaiweka jamii
kwenye nafasi nzuri ya Amani kwa madai kuwa wanahabri wananafasi kubwa katika
jamii ya kuirinda amani,
Kwa
upande wake naye Naibu waziri wa wizara hiyo Anastanzia Wambura amewataka watendaji
wote wa wizara hiyo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili waende sawa na jinsi
Rais Magufuli anavyoenda na kasi ya kuwatumikia watanzania.
WIZARI LUKUVI AKIRIBISHWA WIZARA YA ARDHI,
Waziri,Lukuvi akizungumza na wafanya kazi wa wizara yake |
Waziri
wa Ardhi nyumba na maendelea ya Makazi,William Lukuvi ambaye amerejeshwa tena
kwenye wizara hiyo baada ya uteuzi wa Rais Magufuli,amewataka viongozi wa wizara hiyo ndani ya siku saba
kumpelekea mipango mipya ya kutendaji lasivyo atamfukuza mtendaji ambaye
atashindwa kumpelekea taarifa ya mipango hiyo.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo leo Jijini Dar
es salaam wakati akikaribishwa tena na wafanyakazi wa wizara hiyo mara baada ya
kurejeshwa tena na Rais Magufuli ambapo amesema kwa sasa anataka watumishi wote
wafanye kazi kwa kasi ya Rais Magufuli huku akiwataka mpaka jumatatu wapeleke
taarifa ya mipango kwa kila mtendaji wa wizara hiyo.
Amesema nia ya kuitaji taarifa ya mipango
hiyo ni kutaka kufahamu maeneo yapi muhimu kwa sasa kwa wananchi ili iwe rahisi
kuwatumikia,
Sanjari na hilo Waziri Lukuvi ametoa
kalipia kwa watu wote wanaomiliki mashamba ambayo wameshindwa kuyatekeleza kwa
wakati basi wizara yake itahakikisha mashamba hayo wananyang’anywa na
kurudishwa serikalini kwa ajili ya kupewa watu wengine wenye nia ya kuyatumia
mashamba hayo.
WAZIRI MBARAWA NAYE AANZA NA DAWASCO.
Akiongea na Menejimenti ya Dawasco na Dawasa
ikiwa ni siku
moja tangu kuchaguliwa kwake Waziri wa Maji Mh. Prof Makame Mbarawa alizitaka
Taasisi hizo kuweka mkakati wa lazima utakao hakikisha wateja milioni wanaunganishwa
kwenye mtandao wa Majisafi na salama kwa wakazi wote jijini.
“Tumekuja kutekeleza ahadi ya Rais Magufuli
aliyoitoa
bungeni kuhusu Maji. Aliahidi Serikali ya awamu ya tano pamoja na mambo mengine
watahakikisha wana mtua Mama ndoo kichwani” alisema Mh Waziri.
Ameongeza
kuwa lazima taasisi hizi mbili zijue wajibu wakekwa wananchi na kutekeleza
ahadi ya Rais ili kuwapunguzia wananchi mzigo wakutafuta Maji na hata
wakiyapata gharama zisiwe juu, ameitaka Dawascokuhakikisha inawahimiza wateja
wake wote na taasisi za serikali kulipia Ankaraza Maji kwa wakati.
JAFO NAYE IBUKIA BAYI
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jaffo amewatangazia kihama wakurugenzi
wote nchini watakaoshindwa kuwasimamia wakuu wa idara katika Halmashauri zao.
Naibu huyo alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara
yake ya kikazi ya kwanza ya kushtukiza katika wilaya ya Bahi iliyopo
mkoani Dodoma.
Mbali
na hilo ametoa muda wa siku 27 kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha
zinatumia mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kukusanya mapato katika
halmashauri husika.
Jaffo
amesema kwamba kutokana mfumo wa kizamani wa ukusanyaji mapato unachangia
kwa kiasi kikubwa cha watumishi wengi pamoja na wakurugenzi kufanya ufisadi na
kupiga fedha ya Umma.
Katika
hatua nyingine amewaagiza watumishi wote katika halmashauri ya Bahi pamoja na
halmashauri nyingine nchini kuhakikisha hawakai maofisini na badala yake
watembelee miradi na kujua matatizo ya wananchi.
Amesema
hakuna haja ya watumishi kukaa maofisini kwa ajili ya kusubiri taarifa ambazo
wakati mwingine ni za upotoshaji na kusababisha wananchi kuichukia serikali
yao.
Maoni 1
jafooooo safi sana umeniweka kwako
Chapisha Maoni