Zinazobamba

MAWAZIRI WA MAGUFULI WAANZA KAZI NA MIKWARA,NAPE ANG'AKA KUFUNGIA MAGAZETI,MBARAWA,LUKUVI,JAFFO WALALAMA,SOMA HAPO KUJUA

Waziri wa Habari,utamaduni,Wasanii na Michezo,Nape Nnauye akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo,mara baada kuonyeshwa ofisi yake
 NA KAROLI VINSENT
WAZIRI  wa Habari,Utamaduni,Wasanii na Michezo,Nape Nnauye amewatohu hofu wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini hususani Magazeti pamoja na wanahabari kwa kusema wanaozani kuwa kuchaguliwa kwake na Rais John Magufuli kwenye wizara hio ni kwa ajili ya kuyafungia magazeti,
         Bali amesema hata yafungia magazeti badala yake atahakikisha anakuwa mlezi wa vyombo vya habari pamoja waandishi wa habari ili viweze kufanya kazi kwa weredi.

   Akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya Habari na utamaduni,wasanii na Michezo wakati alipokuwa akipokelewa na wafanyakazi wa wizara hiyo kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kwenye nafasi hiyo na Rais Magufuli ambapo Nape amesema baada ya Rais Magufuli kumchagua kuwa Waziri wa wizara hiyo waliibuka kundi la watu wakisema magazeti yatafungiwa.
   “Nawaomba watu wa sekta ya habari kuondoa dhana ya kwamba mimi nitakuwa mtu wa kuyafungia magazeti,kitu kama hicho akipo kwani nimekuja kwenye wizara hii ili wanahabri wafanye kazi kwa weredi huku mimi nawahahidi nitakuwa mlezi wa vyombo vya habari”amesema Nnauye.

    Amesema nafahamu kwa sasa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 imekuwa ikilalamikiwa sana ila kwa upande wake amedai kuwepo kwa sheria hizo kwa wanahabari kunazidi wavunja moyo wanahabari jambo analilohaidi kulishughulikia
.
      Hata hivyo Nape ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mtama,amewaomba wanahabari pamoja na wamiliki kuhakikisha wanafanya kazi kwa weredi ili kuhakikisha wanaiweka jamii kwenye nafasi nzuri ya Amani kwa madai kuwa wanahabri wananafasi kubwa katika jamii ya kuirinda amani,

     Kwa upande wake naye Naibu waziri wa wizara hiyo Anastanzia Wambura amewataka watendaji wote wa wizara hiyo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili waende sawa na jinsi Rais Magufuli anavyoenda na kasi ya kuwatumikia watanzania.

      WIZARI LUKUVI AKIRIBISHWA WIZARA YA ARDHI,
Waziri,Lukuvi akizungumza na wafanya kazi wa wizara yake
Waziri wa Ardhi nyumba na maendelea ya Makazi,William Lukuvi ambaye amerejeshwa tena kwenye wizara hiyo baada ya uteuzi wa Rais Magufuli,amewataka  viongozi wa wizara hiyo ndani ya siku saba kumpelekea mipango mipya ya kutendaji lasivyo atamfukuza mtendaji ambaye atashindwa kumpelekea taarifa ya mipango hiyo.
    Waziri Lukuvi ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akikaribishwa tena na wafanyakazi wa wizara hiyo mara baada ya kurejeshwa tena na Rais Magufuli ambapo amesema kwa sasa anataka watumishi wote wafanye kazi kwa kasi ya Rais Magufuli huku akiwataka mpaka jumatatu wapeleke taarifa ya mipango kwa kila mtendaji wa wizara hiyo.
     Amesema nia ya kuitaji taarifa ya mipango hiyo ni kutaka kufahamu maeneo yapi muhimu kwa sasa kwa wananchi ili iwe rahisi kuwatumikia,
     Sanjari na hilo Waziri Lukuvi ametoa kalipia kwa watu wote wanaomiliki mashamba ambayo wameshindwa kuyatekeleza kwa wakati basi wizara yake itahakikisha mashamba hayo wananyang’anywa na kurudishwa serikalini kwa ajili ya kupewa watu wengine wenye nia ya kuyatumia mashamba hayo.

   WAZIRI MBARAWA NAYE AANZA NA DAWASCO.


Akiongea na Menejimenti ya Dawasco na Dawasa ikiwa ni siku

moja tangu kuchaguliwa kwake Waziri wa Maji Mh. Prof Makame Mbarawa alizitaka
Taasisi hizo kuweka mkakati wa lazima utakao hakikisha wateja milioni wanaunganishwa kwenye mtandao wa Majisafi na salama kwa wakazi wote jijini.
“Tumekuja kutekeleza ahadi ya Rais Magufuli aliyoitoa
bungeni kuhusu Maji. Aliahidi Serikali ya awamu ya tano pamoja na mambo mengine watahakikisha wana mtua Mama ndoo kichwani” alisema Mh Waziri.
        Ameongeza kuwa lazima taasisi hizi mbili zijue wajibu wakekwa wananchi na kutekeleza ahadi ya Rais ili kuwapunguzia wananchi mzigo wakutafuta Maji na hata wakiyapata gharama zisiwe juu, ameitaka Dawascokuhakikisha inawahimiza wateja wake wote na taasisi za serikali kulipia Ankaraza Maji kwa wakati.  

    

JAFO NAYE IBUKIA BAYI
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jaffo amewatangazia kihama wakurugenzi wote nchini watakaoshindwa kuwasimamia wakuu wa idara katika Halmashauri zao.
Naibu huyo alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara yake ya kikazi  ya kwanza ya kushtukiza katika wilaya ya Bahi iliyopo mkoani Dodoma.
Mbali na hilo ametoa muda wa siku 27 kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatumia mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kukusanya mapato katika halmashauri husika.
Jaffo amesema kwamba kutokana mfumo wa kizamani wa  ukusanyaji mapato unachangia kwa kiasi kikubwa cha watumishi wengi pamoja na wakurugenzi kufanya ufisadi na kupiga fedha ya Umma.
Katika hatua nyingine amewaagiza watumishi wote katika halmashauri ya Bahi pamoja na halmashauri nyingine nchini kuhakikisha hawakai maofisini na badala yake watembelee miradi na kujua matatizo ya wananchi.
Amesema hakuna haja ya watumishi kukaa maofisini kwa ajili ya kusubiri taarifa ambazo wakati mwingine ni za upotoshaji na kusababisha wananchi kuichukia serikali yao.


Maoni 1

Unknown alisema ...

jafooooo safi sana umeniweka kwako