Zinazobamba

WAZIRI MKUU SUMAYE AJIUNGA RASMI NA MAKAMANDA WA CHADEMA,AKUNWA NA FREEMAN MBOWE,SOMA HAPO KUJUA

Sumaye akionyesha Kadi ya Chadema mara baada ya kukabidhiwa 
WAZIRI mkuu Mstaafu wa awamu ya Tatu,Fredrick Sumaye ametangaza rasmi kuhamia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kukabidhiwa na kadi ya uanachama wa chama hicho.Anaandika Mwandishi wetu endelea nayo,

Sumaye ambaye alijiunga na vyama vya Upinzani vinavyounda Ukawa miezi mine iliyopita wakati wa Kampeni za uchaguzi mkuu uliomalizika Octoba 25 mwaka huu,ambapo wakati huo Sumaye alikihama chama cha Mapinduzi CCM na kujiunga na vyama vya upinzani huku akishindwa kusema chama kipi alikiunga nacho.


Sumaye ametangaza hatua hiyo leo Mkoani Arusha wakati wa kuhitimisha Kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Arusha mjini,ambapo amesema amejiridhisha pasio shaka kuwa Chadema ndio chama pekee chenye kuweza kumletea maendeleo Mtanzania jambo lilofanya akihamie chama hicho huku akimpongeza Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kuwa ni
anayeweza kukijenga chama bila kuteteleka

Hakuna maoni