KAMPUNI YA AZAM YAMDINDIA MAGUFULI,NI KUHUSU AGIZO LA SIKU SABA,TRA YAWAANGUKIA WATANZANIA,SOMA HAPO KUJUA
Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi habari (hawapo
pichani) juu ya hatua za ulipaji wa kodi iliyokwepwa katoka katika kontena 329
katika bandari Kavu ya Azam,leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAMPUNI 15 zimeshindwa kulipa kodi za kontena
zilizotoroshwa katika bandari kavu ya Azam inayomilikiwa na Said Salim
Bakhressa na kodi iliyokuwa imekwepwa kwa kampuni 43 ni zaidi ya Sh. Bilioni 12.
Kodi
iliyolipwa ya Kontena 329 hadi jana ambayo ndio ilikuwa ulipaji wa hiari kwa
ndani ya siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ni zaidi ya sh. bilioni 10 pekee.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamisha Mkuu wa Mamlaka
ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo zinatakiwa
kulipa kodi hiyo kwani ulipaji wa hiari wa siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli
umeisha jana hivyo hatua zitachukuliwa kuhakikisha wanalipa kodi hiyo ya
Watanzania.
Mpango
amesema kuwa kampuni 13 tu ndio zimeweza kumaliza kodi yote iliyokuwa
imekadiriwa na TRA kwenye Kontena 329 zilizotoroshwa katika Bandari Kavu ya Azam
(ICD).
Amesema kampuni 15 zimelipa sehemu ya kodi na wanaendelea kuwadai licha
ya kuisha kwa siku saba hivyo wanawajibu kulipa kodi iliyobaki katika Akaunti
ya TRA iliyofunguliwa Benki Kuu (BoT) yenye namba 9921169 785.
Mpango
amesema kuwa wafanyabiashara ambao wameshindwa kulipa katika hicho hatua
zitachukuliwa na wasubiri cha moto.
Amesema watumishi 36 wa TRA wanatuhumiwa kushiriki
katika upotevu wa kodi kutokana na kontena 329 kuondoshwa bandarini
kinyume cha taratibu za forodha na hivyo kusababisha serikali ikose mapato.
Mpango
amesema kuwa TRA inawaomba wananchi taarifa juu mali za kifisadi na mwenendo
mbaya wa baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo.
Amewataka watumishi kuwasilisha tamko za mali
wanazomiliki pamoja na fedha zilizo katika benki na mwisho wa kufanuya hivyo ni
Desemba 15 mwaka huu
Hakuna maoni
Chapisha Maoni