GODBLESS LEMA AMESHINDIKANA ARUSHA MJINI,AZIDI TESA TU,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge Mteule wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa na Aliyekuwa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa |
MGOMBEA Ubunge
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Arusha Mjini, Godblees
Lema ameibuka mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama
vitano vya siasa, Lema amepata kura 68,848 kati ya kura 104,353 zilizopigwa
sawa na asilimia 65.9 akifuatiwa na Mgombea wa CCM, Philemon Mollel aliyepata
kura 35.907 sawa na asilimia 34.4.
Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Navo Mollel
wa ACT-Maendeleo aliyepata kura 342 sawa na asilimia 03, Zuberi Mwinyi wa CUF
aliyepata kura 106, sawa na asilimia 0.1, na Makama Rashidi wa NRA
aliyepata kura 43 sawa na asilimia 0.04.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Juma Iddy,
jimbo la Arusha wapiga kura walioandikishwa ni 317.814, na waliojtokeza kupiga
kura ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 na kura halali ni 104,353.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni