SOKO LA HISA DSE YAWATAKA WANANCHI WACHANGAMKIE HATI FUNGANI YA BENK YA EXIM,SOMA HAPO
Meneja Masoko wa DSE Patrick Mususa wakati wa mkutano na waandishi wa Habari akielezea hali ya mauzo katika soko la hisa, |
SOKO la hisa Mkoani Dar es Salaam,(DSE) limesema hati ya fungani ya hisa iliyowekwa na Benki ya Exim inafikia tamati ndani ya
soko hilo Desemba 8 ya mwaka huu.Aaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam,Meneja wa Mauzo wa DSE,Patrick Mususa amesema hati
hiyo ni bondi iliyowekwa kwenye soko hilo ambapo ilikuwa inawapa fursa ya
wananchi kununua hisa hizo na kujipatia faida la gawio la hisa kwa asilimia 16,
Mususa amesema licha ya mda
kubakiwa mdogo amewataka wananchi kujitokeza kuja kununu hisa hizo,ili waweze
kujiongezea kipato kwa gawio kubwa lilolewekwa na Benki hiyo,
Hata hivo,Mususa amezitaja njia ambazo Wananchi
wanaweza kununua Hisa za Benki hiyo ni kwa kupitia simu ya kiganjani kwa kupiga
namba *150*36# na kufuata maelekezo,
Akizungumzia hali ya soko kwa wiki
iliyopita Mususa amesema mauzo ya soko yameongezeka maradufu tofauti na wiki
iliyopita,
Ambapo katika mauzo hayo benki ya
CRDB ndio imeongoza kwa mauzo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni