KIKWETE AJIABISHA MEDANI YA KIMATAIFA,UBABE UNAOFANYIKA ZANZIBAR WAZIDI MWEKA MSALABANI,SOMA HAPO KUJUA

MGOGORO unaendelea sahivi visiwani Zanzibar umeanza
kumwaibisha Rais anayemaliza mda wake Jakaya Kikwete kwenye medani za kimataifa
baada ya kuonekana sio mtetezi wa demokrasia.Mtandao huu umebaini.Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Duru zinasema kitendo cha Rais Kikwete kumfumbia
macho mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,ZEC,bwana bwana Jecha Salim Jesha kuvunja katiba baada ya kufuta
uchaguzi wote na kutangaza kufanyika tena ndani ya siku 90.
Jecha alitangaza
kuufuta uchaguzi huo wiki iliyopita kwa madai ya uchaguzi huo kutawaliwa na
dosari ambazo anazodai zimepelekea uchaguzi huo kutokuwa na haki.
Licha ya kufuta
uchaguzi huo,jecha ameonekana kufanya maamuzi ya kurupuka kutokana na kutokuwa
na ruhusa kwenye katiba yeyote ambayo inampa mamlaka ya kufanya hivyo,
Taarifa kutoka
Ubarozi wa Marekani ulioko nchini zinasema kitendo cha Rais Kikwete kunyamazia
au kumfumbia macho Jecha kinazidi mweka msarabani Kikwete baada ya kuonekana
ameshindwa kusimamia demokrasia ya kweli.
Rais Kikwete ambaye
amekuwa akijatamba kwenye medani ya kimataifa kwamba ni mtu wa kujali demokrasia
lakini kwa sasa ameshajichafulia kimataifa kwa kuonekana sio mtu wa demokrasia.
Akizungumza na
Fullhabari.blog mwanafunzi wa shahada ya pili ya sayansi ya siasa kutoka chuo kikuu huria cha Tanznaia,Erick Kileo
amesema ni kitendo cha Rais Kikwete kumfumbia macho Jecha kwa kumwacha anakiuka
katiba ya nchi ni jambo linaloweza kuleta machafuko makubwa Zanzibar.
“Ujue nyinyi
mnafikili Jambo hili ni la Mchezo,maana damu itakapomwagika Zanzibar,hakuna
atakayepona kati ya huyo Kikwete na Jecha wake,kwani jambo hili ni baya zaidi
haiwezekana mtu mmoja tu kama jecha anakiuka Katiba ya nchi leo Msimamizi wa
Katiba ambaye ni Rais Kikwete anamnyamazia tu”
Kuchafuka huko kwa
Kikwete kwenye medani ya kimataifa kunakuja ikiwa ni siku tano toka nchi
jumuiya ya ulaya kulaani vikali kitendo cha Jecha kufuta uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa taarifa
kwwa vyombo vya habari zinasema uchaguzi ulifanyika kwa haki na demokrasia
ilikuwepo jambo la kushangaza wanashangaa mwenyekiti huyo kufuta uchaguzi huo.
Taarifa hiyo inasema
Jecha hana mamlaka ya Kikatiba yeyote kufanya hivyo,huku wakimwamulu aendelea
kutangaza matokeo yaliobakia.
Mbali na nchi za
Ulaya kulaani vikali “Ubakaji” huo wa Demokrasia teyari nchi jirani zikiwa zimeshangazwa na kitendo
cha Jecha kufuta uchaguzi huo kwa kusema ni jambo la hatari linaloweza kuleta
machafuko kama yaliyotokea nchini Kenya.
No comments
Post a Comment