MOTO WA MBUNGE SAED KUBENEA WAANZA KUITISHA CCM,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Mbunge Mteule wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akikabidhiwa cheti na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hil |
BAADHI ya
wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameonekana kuwa na wasiwasi kwa kitendo
cha Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea
kupenya katika uchaguzi mkuu na kuingia bungeni. Anaandika Dany Tibason, Mpwapwa … (endelea).
Kwa
masharti ya kutokutaka kutajwa majini makada hao walisema kuwa kutokana na
umahili wake wa kufanya kazi kubwa ya kiuchunguzi ni wazi kuwa ataweza kuiumbua
serikali hasa katika mijadala mbalimbali.
“Akiwa katika
kipindi chake cha uandishi alikuwa akiandika habari za uchambuzi na uchunguzi
kwa kina na sasa kaingia bungeni hakika kutachimbika,” walisema makada hao.
Wakati huo huo baadhi ya wananchi wa Mpwapwa wameonesha furaha
yao kwa ushindi wa Mbunge mteule wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule (Chadema)
maarufu kwa jina la Prof J.
Kwa nyanati tofauti
wananchi hao wamesema kitendo cha nguli huyo wa mziki wa kizazi kipya kujitosa
katika siasa ni ukombozi kwa vijana wenye vipaji mbalimbali.
Mmoja wa wananchi
ambaye alizungumza na gazeti hili, Hawa Makau amesema mwimbaji huyo wa mziki wa
kizazi kipya ni kati ya wanamuziki ambao wanajitambua.
Hawa amesema kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa jimbo la Mikumi
limepata mbunge ambaye kwa vyovyote vile ataweza kuinua vipaji vya wasanii
wadogo na wakiunganisha nguvu yeye na Joseph Mbilinyi wataweza kupigania
maslahi ya wasanii.
Naye Angela Mayoba amesema kitendo cha wanamuziki hao kuingia
katika Bunge iwe chachu ya kukuza na kutetea maslahi ya wanamuziki wa nyimbo za
injili pamoja na muziki mbalimbali.
Hata hivyo amesema umefika sasa wa jamii na wasanii wenyewe
kujitambua na kuacha vitendo vya kutumia majukwaa kwa kujidhalilisha na badala
yake watambue kuwa ni kazi kama ilivyo kazi nyingine ambayo inamjengea mtu
heshima kama ilivyo kwa Joseph Haule na Sugu.
No comments
Post a Comment