NGOMA BADO MBICHI ZANZIBAR.ZEC YAZOMEWA KILA KONA,NI KWA UBAKAJI WAKE WA DEMOKRASIA,SOMA HAPO KUJUA

BAADHI ya
viongozi wa vyama vya siasi nchini wameshauri kuundwa kwa serikali ya mpito
itakayoshirikisha kila chama kufuatia mgogoro wa kufutwa matokeo ya Zanzibar. Anaandika Faki Sosi …
(endelea).
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya Mkutano wa Baraza la Vyama
vya Viasa wa kumuaga Rais Jakaya kikwete anayemaliza muda wakewamesema kuwa, ni
vema serikali hiyo ikahusisha zaidi ya chama kimoja cha upinzani.
Mgombea Urais
visiwani Zanzibar kupitia ADA TADEA, Juma Ally Hatibu ameshauri Rais Kikwete
kuuvalia njuga mgogoro wa Zanzibar kutokana na kwamba unaweza kukuwa endapo
katiba ya visiwa humo itapaoshindwa kufuatwa.
“Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar imeboronga na haikuwajibika ipasavyo ndio sababu ya kuliingiza taifa
kwenye mgororo huu,” amesema Hatibu.
Mwenyekiti wa Chama
cha Wakulima (AFP) ambaye alikuwa mgombea urais wa chama hicho visiwani
Zanzibar, Sudi Said Sudi amesema kuwa, kipindi hiki ambacho nchi ipo kwenye
mchakato wa kusubiri kurudiwa kwa uchaguzi, iundwe Serikali ya Mpito.
Amesema serikali
hiyo haipaswi kuwa ya vyama viwili au kimoja cha siasa, hata hivyo ameridhia
kufutwa kwa uchaguzi huo kutokana kwa madai ya kasoro zake.
“Mimi kwa upande
wangu nimeona kuwa uchaguzi ulikuwa una mapungufu mengi ikiwa kuna watu ambao
wamekutwa wakiwa wana kura feki, kupigana kwa wajumbe wa ZEC pia kuonekana kwa
watu ambao si mawakala wala si wasimamizi wa uchaguzi ndani ya vituo,” amesema
Sudi.
Mwenyekiti wa
Chama Cha Demokrasia Makini, Muhammedi Abdullah amesema kuwa, kwa mujibu wa
katiba kifungu cha 28(1) kinaeleza kwamba ukumo wa Rais kutoka madarakani ni
mpaka rais mpya aapishwe.
Ameshauri kuwa rais
aliyekuwepo madarakani hatakiwi kuondoka mpaka apatikane rais mwengine.
Kwa upande wake
aliyekuwa Mgombea urais wa Chama cha TLP, Maximullan lyimo amesema kuwa
ameshindwa ambapo ameitaka serikali mpya kuunda serikali isiyokuwa na itikadi
ili kujileta maendeleo katika taifa.
Mkutano huo
uliandaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kupitia Baraza la Wanasiasa nchini.
MAALIM
SEF SHARRIF HAMAAD ANENA
HUKU hali ya
mambo hapa Zanzibar ikiwa haijatulia, Maalim Seif Shariff Hamad leo amesema
mgogoro uliosukumwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha
Salim Jecha utatatuliwa kwa njia za kisiasa wala sio kiulinzi kama inavyojengwa
taswira. Anaandika Jabir Idrissa, Zanzibar …
(endelea)
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu
ya Chama cha Wananchi (CUF) Mtendeni mjini hapa, Maalim Seif ambaye ni Katibu
Mkuu wa chama hicho na mgombea urais wa Zanzibar, amesema kuwepo kwa askari
wengi wa vikosi mbalimbali nchini hakutasaidia kwa lolote kwani suala lililopo
ni la kisiasa linalohitaji kutatuliwa kwa mujibu wa sheria.
“Ni kweli unavyosema kuna maaskari wengi mitaani. Nami nashangaa
lakini najua kwamba tuna tatizo la kisiasa linalopaswa kutatuliwa kisheria kwa
kurudi kwenye msingi wa sheria na wala wananchiu wasidanganywe kuwa kuna njia
nyingine,” amesema.
Maalim Seif alikuwa ameulizwa kwamba inakuaje anaendelea kuwapa
matumaini wana-CUF na wananchi wa Zanzibar kuwa jitihada kubwa zinazofanywa na
watu mbalimbali katika kutatua mgogoro uliotokea kuhusu matokeo ya uchaguzi
kufutwa na Mwenyekiti Jecha, wakati ndani ya nchi wanaonekana maaskari wengi
wakiwa na silaha nzito kama vifaru hadi kisiwa Pemba.
Amesema Rais Jakaya Kikwete ana dhamana ya kubeba katika hali
iliyopo kwa kuwa ndiye pia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
Kwamba kama wananchi wanakuta maaskari wengi wenye silaha nzito, alisema, basi
mtu hatakosea akisema na kuamini kuwa ni yeye Rais Kikwete anayeamrisha kuwepo
kwa maaskari hao.
Akizungumzia jitihada zinazofanyika kutatua mgogoro, Maalim Seif
alisema kwa kadri anavyojua, kuna matumaini makubwa ya kupatikana mafanikio ya
jitihada hizo katika “Siku chache zijazo.” Alisema matatizo yaliyotokea
yamesababishwa na kikundi kidogo tu cha watu wanaomsukuma Dk. Ali Mohamed Shein
kwenda kwenye njia wanayoitaka wao ambayo aliita kuwa ni “inayojali maslahi yao
binafsi wala si maslaha makubwa ya Wazanzibari.”
Maalim Seif amesema ameambiwa kwamba Mwenyekiti Jecha amerudi
kazini na kuitisha kikao cha Tume ya Uchaguzi Zanzibar huku akilazimisha
kushawishi makamishna wa tume hiyo kumuunga mkono katika msimamo wake wa
kuyafuta kinyemela matokeo ya uchaguzi akiwa ameshatangaza matokeo ya majimbo
32 kati ya 54 ya Zanzibar.
“Anahangaika bure huyu Jecha kwa sababu ameshindwa kutambua
kwamba alichoota kukifanya ni kitu haramu kisichoungwa mkono na kifungu
chochote cha Sheria ya Uchaguzi Na. 11 ya 1984 wala Katiba ya Zanzibar ya mwaka
1984. Msimamo wetu uko wazi kwamba tunataka Tume ifanye kazi yake, ikamilishe
kuyatangaza matokeo ya kura zilizobaki na kumtangaza mshindi wa urais. Hapo
itakuwa imewajibika,” alisema.
Maalim Seif amesema amekuwa akisisitiza kuwa uongozi atakaounda
hautalipiza kisasi kwa mtu yeyote kwa sababu tayari siasa za kulipizana visasi
zilishafutwa kufuatia kutandikwa kwa siasa za maridhiano zilizotokana na
jitihada zake na Rais Mstaafu Amani Karume.
Katibu Mkuu wa CUF ambaye juzi aliweka muda wa saa 48 wa
kutafutiwa ufumbuzi mgogoro wa uchaguzi uliotokana na uamuzi wa Mwenyekiti
Jecha wa peke yake kufuta uchaguzi wote, amesema kwa kuwa anaridhika na
jitihada zinazofanywa na kuutatua mgogoro, angali anaasa wananchi watulie na
wasijihusishe na vitendo vya kuvunja sheria.
Mapema leo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,
Mohamed Aboud Mohamed alitoa taarifa kupitia Shirika la Utangazaji la Zanzibar
(ZBC) kwamba serikali inaunga mkono uamuzi wa Tume na kutaka wannchi watulie
kusubiri hatua inayofata ya tume
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment