Zinazobamba

WANAOMTETEA LOWASSA,WAJIBU MASWALI HAYA,SOMA HAPO KUJUA



MASWALI MAGUMU KWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASA 
1.Tangu umejiuzulu nafasi yako ya uwaziri mkuu kufuatia kashfa ya ufisadi wa Richmond, imekuchukua miaka 7 kujitetea mbele ya umma.Ulikua wapi muda wote huo?
        2.Umelieleza taifa na dunia kuwa hukufanya kazi sehemu yoyote zaidi ya CCM tangu mwaka 1977, Je utajiri ulionao umeutoa wapi? Huko CCM kuna biashara gani ulifanya?
       3.Kwanini hajawahi na inaonekana huwezi kukemea wala kuzungumzia Rushwa na ufisadi?
         4.Kwanini sehemu kubwa ya wanaokuunga mkono ni wale ambao walifeli au kukataliwa na wananchi au kufukuzwa kazi katika nafasi mbalimbali za chama na serikali kwa kashfa? Mfano Rostam Azizi, Nazir Karamagi, Andrew Chenge, Lawrence Masha, Juma Kapuya, Cyril Chami n.k?
        5.Ulizipataje hisa zako unazomiliki VODACOM? Ulizinunua lini na kwa kiasi gani?
         6.Wakati unaajiriwa na CCM kama katibu msaidizi miaka ya 70, inasemekana ulimuibia baba yako mzazi ng'ombe ukawauza na kununua gari, kisha mzee wako akaenda kukushitaki kwa viongozi wa Chama kuwa hufai na ufukuzwe kazi. Je, hii ni kweli?
         7.Wewe ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa, kikao kinachojadili na kuamua mambo makubwa ya kusimamia serikali inayotawala. Je,umewahi kujenga hoja zipi za kutetea wananchi? Kusimamia serikali? Mara ngapi? Lini?
        8.Tangu umekua mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje miaka mitano sasa, wewe ni mwenyekiti pekee ambae hujawahi kusimama hata mara moja kusoma taarifa ya kamati bungeni. Je, ni kwanini? Tatizo ni afya yako inakufanya usiweze kusimama kuongea kwa muda mrefu au nini?
        9.Kwanini unatumia pesa nyingi sana kutafuta urais wa nchi? Pesa hizo utazirudishaje kwa hao unaowaita marafiki zako? Ikulu kuna biashara gani? Je, ikiwa Urais unanunuliwa, sisi watoto wa masikini watoto wetu wajifunze nini? Kuwa wataendelea kubaki katika tabaka la watawaliwa hadi watakapokuwa na mabilioni ya kutosha?

          10.Kumbukumbu zinaonesha kuwa hayati mwalimu Julius Nyerere aliwahi kukukataa kutokana na kuonekana ukiwa na ukwasi usio na maelezo,Je, uliwahi kumjibu mwalimu kabla ya umauti wake kuwa ulipataje mali zako? Ili arekebishe kauli yake? 
Tuko Sawa Sawa jamani

Maoni 4

Bila jina alisema ...

ACHA KUPOST PUMBA WEWE MTU MZIMA.

Bila jina alisema ...

MTU MZIMA UNAPOST UTUMBO

Bila jina alisema ...

Wewe unataka rais gani kama ulichopost si utumbo. Lowasa ni jembe ndani ya CCM. Hatutaki rais maskini tuchague rais ambaye ni tajiri kama Lowasa. Rais maskini atauza nchi na kufikiria jinsi ya kuwatajirisha ndugu zake.

Unknown alisema ...

Hatuchagui pesa tafadhalini sana ccm imetukandamiza sana miaka kumi imepita ktk uongozi wa JK hakuna kingine tunaogea zaidi ya ufisadi kodi yako na mm tuwewanjanja tafadhali