Zinazobamba

EXCLUSIVE-PROFESA LIPUMBA AMLIPUA LOWASSA,KINGUNGE,AMTAKA HOSEA WA TAKUKURU KUMCHUNGUZA LOWASSA MARA MOJA SOMA HAPO KUJUA

Pichani ni Profesa Lipumba akizungumza jambo
 na wandishi wa Habari picha na maktaba
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba ni kama amemshukia Edward Lowassa ambaye ni miongoni mwa Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM ambao wanautaka urais kwa Udi na Uvumba kwa kusema ni Mtu hatari ambaye watanzania wanatakiwa kumwogopa.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
       Vilevile Profesa Lipumba amemshukia pia Mwanasiasa Mkongwe nchini Kingunge Kombale Mwiru na kusema amemsaliti Mwalimu Julias Nyerere kwa kuwashabikia watu mafisadi.
         Hayo yamesemwa na Profesa Lipumba leo Jijini Dar es Salaam Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Profesa lipumba amemtaka Mkurugenzi wa TAKUKURU Edward Hosea kumchunguza mara moja Edward Lowassa kwa hatua yake ya awali aliyotangaza nia kwa kusema ametumia pesa nyingi huku akionyesha wazi yeye ni mtumishi wa umma.
       “Mimi nashangaa sana ofisi ya Hosea kuwa kimya kwa watu kama wakina Lowassa,ambao kutangaza nia tu wametumia ghalama kubwa huko tunajua wazi hawa ni watumishi wa Umma wasiku nyingi pesa hizi wanazitoa wapi za kukodi mamia ya watu toka mikoa mbalimbali na kuwalipa posho kubwa sana, sasa huyu mtu pesa katoa wapi na atazirudishaje?watanzania wawe makini sana”amesema Profesa Lipumba.
        Profesa Lipumba ameongeza kuwa  kwa kusema hata  Watangaza nia ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM kutumia pesa nyingi imeonyesha wazi kwamba walifanya makusudi  “kunyofoa”Maoni ya Wananchi kwenye Katiba pendekezwa ambayo iliwabana watumishi wa Umma kutangaza mali zao zote.
     “Hawa wakina lowassa pamoja na wenzake walitumia nguvu kubwa kuzika maoni ya wananchi kwenye katiba ile husasani kwenye kipengele ambacho kinawataka Viongozi kutangaza mali zao pamoja na pesa  wanazomiliki kabla ya kuwania sehemu mbali mbali za uongozi,kumbe  walikuwa wanamalengo haya”ambainisha Profesa lipumba.
    KUHUSU SUALA LA KINGUNGE.
Profesa Lipumba ambaye ni Gwiji wa masuala ya uchumi  Dunia ameonyesha masikitiko yake kwa Mwanasiasa Mkongwe kutokana ndani ya CCM kingunge Kumbale Mwiru kitendo chake  cha kwenda Arusha kwenye Mkutano wa Hadhala uliondaliwa na Edward Lowassa wenye ajenda ya kutangaza safari ya matumaini.
Ambapo Lipumba amesema Mwanasiasa huyo amemuongusha Mwalimu Nyerere ambaye ni mtu mtetezi wa Masikini.
“Hivi naweza kusema Mzee mwezangu Kingunge hizi ni njaa au sijui ?maana namjua Kingunge huyo kwenye miaka ya 1970 alikuwa anakuja na kunadi Sera za Ujamaa na kujitegemea,hivi hizi sera za kuwa upande wa Mafisadi ni ndio Ujamaa wa Karne ya 21 ua?”amehoji Profesa Lipumba.
Katika hatua nyingine Chama hicho cha CUF ambacho kinaunda Umoja wa Vyama vinavyounda UKAWA wameipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utalawa Bora ambayo ilitoa Ripoti kuhusu tukio lilitokea Januari mwaka huu kwa wafuasi wa Chama hicho  ambao  walikuwa wakienzi kumbukumbu ya Miaka 16 ya kifo cha Wananchama wake kiliochotokea 2001 Visiwani Zanzibar.
  Ambapo kwa mujibu wa Ripoti hiyi ilionyesha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kuwapiga wananchama hicho huku ikivunja kanuni za Vyama vya Siasa nchini,kwa mujibu wa Lipumba anasema Ripoti hiyo wao  wameipokea kwa moyo mmoja na wameitaka Serikali kufanyika kazi mapendekezo yake.


Hakuna maoni