Zinazobamba

BUNGE LIMESITISHWA GAFLA,NI BAADA YA MSIBA MKUBWA,SOMA HAPO KUJUA

BUNGE TZ.
BUNGE la Jumuhuri wa Muungano limesitisha Shughuli zake za kusoma bajeti mbali mbali za wizara mpaka tarehe 4 mwezi huu kutokana na Msiba wa Mbunge wa  Jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa CCM,anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Kwa Mujibu wa Taarifa ilitolewa na Ofisi ya Bunge inasema wamesitisha kazi zote za Bunge ili kupisha taratibu zengine za kibidamu.ikiwemo Mwili wa Marehemu kuagwa kesho tarehe 3 Juni 2015 kuanzia saa 4 asubuhi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, na baadaye mwili kupelekwa nyumbani kwake Ukonga, Dar es Salaam
    Mbunge Mwaiposa kifo chake kimetokea majira  ya saa nne asubuhi mjini Dodoma Bungeni.

Ambapo sababu ya Kifo chake kinatokana na kusumbuliwa na Ugonjwa na Shinikizo la Damu,taarifa za awali zinasema amefariki kwenye Hoteli jirani kituo cha mafuta Ahabiby,

Hakuna maoni