WANAOMTETEA LOWASSA,WAJIBU MASWALI HAYA,SOMA HAPO KUJUA
MASWALI MAGUMU KWA MH.
EDWARD NGOYAI LOWASA
1.Tangu umejiuzulu nafasi yako ya uwaziri mkuu kufuatia kashfa ya ufisadi wa Richmond, imekuchukua miaka 7 kujitetea mbele ya umma.Ulikua wapi muda wote huo?
1.Tangu umejiuzulu nafasi yako ya uwaziri mkuu kufuatia kashfa ya ufisadi wa Richmond, imekuchukua miaka 7 kujitetea mbele ya umma.Ulikua wapi muda wote huo?
2.Umelieleza taifa na dunia kuwa
hukufanya kazi sehemu yoyote zaidi ya CCM tangu mwaka 1977, Je utajiri ulionao
umeutoa wapi? Huko CCM kuna biashara gani ulifanya?
3.Kwanini hajawahi na inaonekana huwezi
kukemea wala kuzungumzia Rushwa na ufisadi?
4.Kwanini sehemu kubwa ya wanaokuunga
mkono ni wale ambao walifeli au kukataliwa na wananchi au kufukuzwa kazi katika
nafasi mbalimbali za chama na serikali kwa kashfa? Mfano Rostam Azizi, Nazir
Karamagi, Andrew Chenge, Lawrence Masha, Juma Kapuya, Cyril Chami n.k?
5.Ulizipataje hisa zako unazomiliki
VODACOM? Ulizinunua lini na kwa kiasi gani?
6.Wakati unaajiriwa na CCM kama katibu
msaidizi miaka ya 70, inasemekana ulimuibia baba yako mzazi ng'ombe ukawauza na
kununua gari, kisha mzee wako akaenda kukushitaki kwa viongozi wa Chama kuwa
hufai na ufukuzwe kazi. Je, hii ni kweli?
7.Wewe ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
CCM taifa, kikao kinachojadili na kuamua mambo makubwa ya kusimamia serikali
inayotawala. Je,umewahi kujenga hoja zipi za kutetea wananchi? Kusimamia
serikali? Mara ngapi? Lini?
8.Tangu umekua mwenyekiti wa kamati ya
bunge ya mambo ya nje miaka mitano sasa, wewe ni mwenyekiti pekee ambae
hujawahi kusimama hata mara moja kusoma taarifa ya kamati bungeni. Je, ni
kwanini? Tatizo ni afya yako inakufanya usiweze kusimama kuongea kwa muda mrefu
au nini?
9.Kwanini unatumia pesa nyingi sana
kutafuta urais wa nchi? Pesa hizo utazirudishaje kwa hao unaowaita marafiki
zako? Ikulu kuna biashara gani? Je, ikiwa Urais unanunuliwa, sisi watoto wa
masikini watoto wetu wajifunze nini? Kuwa wataendelea kubaki katika tabaka la
watawaliwa hadi watakapokuwa na mabilioni ya kutosha?
10.Kumbukumbu zinaonesha kuwa hayati
mwalimu Julius Nyerere aliwahi kukukataa kutokana na kuonekana ukiwa na ukwasi
usio na maelezo,Je, uliwahi kumjibu mwalimu kabla ya umauti wake kuwa ulipataje
mali zako? Ili arekebishe kauli yake?
Tuko Sawa Sawa jamani
Tuko Sawa Sawa jamani
Maoni 4
ACHA KUPOST PUMBA WEWE MTU MZIMA.
MTU MZIMA UNAPOST UTUMBO
Wewe unataka rais gani kama ulichopost si utumbo. Lowasa ni jembe ndani ya CCM. Hatutaki rais maskini tuchague rais ambaye ni tajiri kama Lowasa. Rais maskini atauza nchi na kufikiria jinsi ya kuwatajirisha ndugu zake.
Hatuchagui pesa tafadhalini sana ccm imetukandamiza sana miaka kumi imepita ktk uongozi wa JK hakuna kingine tunaogea zaidi ya ufisadi kodi yako na mm tuwewanjanja tafadhali
Chapisha Maoni