MGOMO GAZETI LA CCM,MAPYA YAFICHUKA,KIGOGO WA CCM ATAJWA KUFANYA UFISADI SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Pichani ni Katibu mkuu wa ccm bwana kinana |
HATIMAYE
siri zimeanza kufichuka juu ya Mgomo mkubwa wa Wanyakazi wa Gazeti la Uhuru
baada ya kubainika Bodi ya watendaji wa
Gazeti hilo kukumbatia Ufisadi ambao umepelekea Wanyazakazi wake kukosa Mshahara unaofikia miezi mitano
sasa.Mtandao huu umebaani.Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Gazeti la
Uhuru ambalo linamilikiwa na Chama cha Cha Mapinduzi CCM lilianzishwa kwa lengo
la kueneza Propaganda za chama hicho kwa watanzania pamoja na kuviponda vyama
vya upinzani nchini,limekubwa na mgomo mkubwa wa Wafanyakazi ulioanza jana huko
wakidai kuteseka kwa kukosa mishahara pamoja na malupulupu kwa mda wa miezi
mitano.
Kwa mujibu wa Chanzo chetu kilichopo
ndani ya Gazeti hilo kimeuambia mtandao huu kwamba sababu ya Mgomo huo
unatokana na Mwenyekiti wa Bodi la la Gazeti hilo aliyekuwa Mstahiki meya Adam
Kimbisa kuitisha kikao cha Bodi haraka na kumsimamishwa Mkurugenzi wa Gazeti la
Uhuru bwana Piter Kilangwa bila sababu ya msingi.
Bwana Piter Kilangwa ambaye kabla ya kuja
Gazeti hilo alikuwa Mhariri wa Magazeti ya Serikali na aliteuliwa nafasi hiyo
na Kigogo wa Juu wa CCM kwa lengo la kulikuza Gazeti hilo kimaudhui ambayo yanadaiwa kuwa yalishuka.
Kwa Mujibu wa Mtoa taarifa huyo amesema
kilichofanywa na Bodi ya Uhuru Gazeti cha Kumsimamisha Bwana Kilangwa ni kutaka
kuficha madudu ya Kifisadi yanayofanywa na Katibu mkuu wa Bodi hiyo kwenye matangazo mbali mbali yanayoletwa
Gazetini huku akishilikiana na watendaji wachache wa Gazeti la Uhuru.
“Sikiliza
nikwambia hapa wafanyakazi tumegoma kushinikiza Bwana Kilangwa arudi maana huyu
alikuwa ameanza kubaini sababu ya sisi kutolibwa mshahala kwa miezi mitano
kwamba inatokana na Katibu wa Bodi kushirikiana na watendaji wa bodi kutafuna
pesa za matangazo yanayotoka wizara mbali mbali huku sisi tukisota”
Ameongeza kuwa kwa kusema “ Bodi ya uhuru
baada ya kuona bwana Kilangwa ameanza kubaini michezo michafu ya kifisadi ya
kuiba pesa za matangazo kutoka serikali wakamsimamisha kazi ili madudu hayo
yasifichuke,achia hivyo bwana huyo alikuwa ameanza kuwatetea wafanyakazi ambao wamekuso
mshahala kwa siku chingi huku akuna sababu ya msingi”
Mbali na hujuma Matangazo,sababu inayotajwa
huenda imepelekea gazeti hilo kuyumba ni kutokana na kushuka kwenye maudhui
yanayozalishwa.
“Ujue sahivi
kazi ya Magazeti imekuwa na ushindani mkubwa,ujue hilo gazeti limeshuka sana
kimaudhui yaani likuwa kama jarida la CCM,lipo kwa ajili ya kuwaponda UKAWA na
kuwasafisha watuhumiwa wa Ufisadi wa CCM ambao ndio wamelimaliza Ta9ifa hili. Wewe
unategemea nini mwananchi atalisoma gazeti hili ndio maana limeshuka”

No comments
Post a Comment