HABARI KUBWA LEO-WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI WAIAPIA SERIKALI YA KIKWETE,WASEMA NYAKATI ZA KUOGOPANA ZIMEPITWA,SOMA HAPO KUJUA
| Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari hivi karibuni Dar es Salaam , kuhusu mswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao ulitaka kuwasilishwa bungeni kwa dharula. Kulia ni Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi. |
WAMILIKI wa
Vyombo vya Habari nchini wametishia kutozitangaza Habari zozote zinazohusu
Serikali ya Chama cha Mpinduzi CCM endapo Wabunge watapitishwa Mswaada wa
kuvibana Vyombo vya Habari wa mwaka 2015.Mtandao huu umetaarifiwa Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Mswaada huo
wa vyombo vya Habari ambao unatarajiwa kusomwa kwa mara ya pili Bungeni kwa
hati ya Dharula na kujadiliwa harafu kupitishwa ndani ya Siku kumi ziliobakia
kabla ya Rais Jakaya Kikwete ajalivunja Bunge hilo tarehe 9 mwezi ujao,unatajwa
na Wamiliki hao endapo ukupitishwa mswaada huo na kuwa sheria basi ndio utakuwa umeizika tasnia ya Habari nchini.
Pia Sababu hiyo inatokana na Mswaada huo
na Vipengele vikali kwa Waandishi wa Habari na kupelekea kuunyima uhuru kwa
kupata habari ambao mara kwa mara Serikali imekuwa ikijinadi ndio imetoa uhuru
huo.
Akizungumza na Mtandao huu Ummiliki moja
wa Gazeti ambae akutaka jina lake liaandikwa kwenye Mtandao huu amesema kwa
sasa wamiliki hao, hawatakubali kupelekeshwa na Serikali endapo watapitishwa Mswaada
huo ambapo ni kandamizi kwenye Sekta ya Habari nchini.
“Sisi tunajua tunafayiwa mchezo mchafu hapa
maana kamati ya za Bunge zimesema mswaada huo hautapelekwa Bungeni ila
kunataarifa tumezipata kwamba ni danganya toto na lazima upelekwe mswaada huo ,na
wataupitishwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi CCM,sasa nawaambia wao wakimwaga
mboga na sisi tunamwaga Ugali,nakuhakikishia hatutaandika Habari zinazohusu
Serikali ya CCM”amesema Mmiliki huyo ambaye ni mujumbe wa (MOAT)
Ameongeza kwa kusema kuwa “Hii Serikali
tumeivulia sana,wametunga sheria za Hovyo kama ile ya Takwimu ya 2015 na Uharifu
wa mitandao, tumewavumilia nakwambia
sasa uvumilivu ndio basi maana wameua mashirika ya Umma sasa wanakuja hadi kuua
sekta ya binafsi kwa kutunga sheria mbaya kama hizi,sasa wewe utaona ndio
utajua na sisi tunanguvu hapa nchini”
Taarifa ambazo mtandao huu umezipata
zinasema Shinikizo la Mswaada huo kupelekwa haraka Bungeni na kupitishwa
unasukwa na Waziri mmoja Mwandamizi wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ambaye mara
kwa mara amekuwa akiwabeza waandishi wa Habari nchini.
“Huyu bwana
(anamtaja)anashikilia bango kweli mswaada huo upelekwe Bungeni haraka sana
maana anahasira ya waandishi wa Habari,kwakuwa kipindi cha nyuma aliindikwa
Vibaya mpaka akagombana na viongozi wa Dini na anasema sababu ya kushuka
kisiasa basi waandishi wa Habari wamepelekea
kushuka kwake kisiasa”amesema Mpashaji huyo wa mtandao huu.
Waziri
huyo Mwandamizi ambaye ni miongoni mwa Mkada wa CCM waliotangaza nia na sasa
yuko kwenye mikoa mbali mbali akitafuta wadhamini ni miongoni mwa watu
wanang’ang’ani mswada huo kupelekwa bungeni bila kuangalia athari zake kwa
Sekta ya Habari nchini na Duniani.
Mpaka kufikia juzi Jukwaa la Wahariri
pamoja Baraza la Habari nchini (MCT) walikuwa mkoani Dodoma wakiongea na Kamati
mbali mbali kuangalia uwezekano wa kuundoa mswaada huo ambao haujawai tokea
Dunia.
Mbali na
Watetezi hao wa Habari kuwepo Dodoma,inakuja ikiwa ni Teyari Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Freeman Mbowe kutangaza
kuanzisha Fujo Bungeni endapo Serikali ikipeleka Mswaada huo kwa kusema Bunge
halitakalika
1 comment
Habari yenyewe ni nzuri na muhimu sana kwa jamii. Ila imejaa makosa mengi ya kisarufi. Naomba mwandishi ajaribu pia kuzingatia matumizi ya Kiswahili sanifu.
Post a Comment