HABARI KUBWA LEO-BAJETI MBOVU YAPITA,WASAKA URAIS WAWAGEUKA WATANZANIA SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akipiga kura ya ndio wakati bunge lilipokuwa likipitisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Bungeni mjini Dodoma leo. Kulia ni Mbunge wa Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Diana Chilolo. |
BAJETI ya Serikali
kwa Mwaka wa Fedha 2015/16 imepita kwa zaidi ya asilimia 80, hata hivyo
malalamiko ya wabunge wameendelea kutawala. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Sehemu kubwa ya malalamiko kwa baadhi ya
wabunge yaliitaka serikali kuangalia upya uamuzi wa kungeza kodi kwenye Mafuta
ya Taa, Dizeli pamoja na Petroli.
Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Saada
Mkuya alisema kuwa, ni lazima wananchi watoe fedha hiyo ili kurahisisha huduma
ya umeme kusambaa vijijini.
Akizungumzia lalalamiko ya wabunge
kuhusu ongezeko la tozo ya Mafuta ya Taa, Petrol na Dizel amesema, hakuna jinsi
ya kukwepa tozo hiyo.
“Hatuwezi kuikwepa tozo hiyo kwani
tunahitaji Sh.100 kwa kila lita moja na fedha hiyo ikikusanywa zinaweza
kupatikana Sh. bilioni 276 kutokana na tozo ya mafuta kwa kila lita.
“Katika fedha hizo biloni 90
zitaelekezwa katika mfuko wa maji vijiji ili kuweza kuwapatia wananchi wa
vijiji huduma hiyo ya maji kwa urahisi,” amesema Mkuya.
Amesema, hakuna njia yoyote wala
miujiza yoyote ya taifa kuwa na maendeleo kama haitakuwa tayari kutumia kodi
zake katika kufanya shughuli za maendeleo.
“Ni lazima wananchi wakachangia
fedha hiyo ya Sh.100 na fedha hiyo tunaihitaji sana, hakuna njia ya kuweza
kukwepo na lazima inapotokea changamoto yoyote wakati mwingine ichukuliwe kama
fursa kwa sasa matumizi ya mafuta ya taa yamepungua.
“Lakini tukiweza kusambaza umeme wa
kutosha jiijini hiyo ijulikane kuwa ni biashara kwani siyo kwa ajili ya kuwasha
taa tu, bali ni kuweza kuutumia umeme huo kufanya shughuli mbalimbali za
uzalishaji,” amesema Mkuya.
Hata hivyo, baada ya wabunge kupiga
kelele kwa kuitaka serikali iongeza pensheni kwa wazee wastaafu, sasa serikali
imekubali kuongeza pensheni kutoka Sh. 85,000 iliyokuwa imependekezwa na kufika
Sh. 100,000.
Waziri Mkuya alitoa kauli hiyo
alipokuwa akihitimisha mjadala wa siku saba wa kujadili Bajeti Kuu ya Mwaka wa
Fedha 2015/16.
Na kwamba, serikali imekubali
kuwalipa pensheni wazee wote nchini bila kujali kama walikuwa watumishi wa
serikali.
Mkuya amesema, serikali imetenga
fedha kwa ajili ya maofisa na watafanya uhakiki wa wazee hao ili kuweka
miundombinu rafiki ambayo itawawezesha kulipwa fedha hizo.
Utaratibu ukikamilika amesema, wazee hao
watatakiwa kulipwa kiasi cha Sh. 10,000 kwa mwezi ambapo kwa idadi ya sasa ya
sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, ni wazee milioni 1.2 ambao watalipwa
Sh.10,000 sawa na Sh. Bilioni 140 kwa mwezi.
Akiendelea kujibu hoja za wabunge
wengi walilalamikia kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma amesema, mpaka
sasa wamebaini kuwepo kwa upotevu wa Sh. Bilioni 6 ambazo watumishi wa serikali
kwa kushirikiana na wafanyakazi wa mabenki zimekuwa zikilipwa kama mafao ya
wastaafu.
Akizungumzia kuhusu masuala ya uchumi
amesema, ni kweli uchumi unaonekana kupanda lakini hali halisi ya Watanzania
bado hawajaweza kuona uhalisi wa uchumi huo.
Akizungumzia kigezo cha serikali kukua
kwa uchumi ni katika upatikanaji wa huduma za jamii kwa ujumla wake.
Amesema, kwa miaka mitano mfulilizo
umasikini umepungua kwa asilimia 6.2 jambo ambalo linaonesha kuwa, zipo juhudi
za makusudi za kupambana na umasikini.
Kuhusu matumizi ya Dola za
Marekani Mkuya amesema, serikali bado
inahitaji kuwa na dola za kutosha ambazo zitakuwa zimethibitiwa.
Amesema, kwa sasa
Watanzania wanaishi kwa dola 1060 kwa mwaka na kuna upungufu wa dola 30 ili
kufikia uchumi wa kati.
Kwa hisani
ya Mwanahalisi oline

No comments
Post a Comment