Zinazobamba

BWANA RAYMOUND MUSHI AWAPA SOMO DAWASA,SOMA HAPO KUJUA

 
Translate message



Viongozi Mbali mbali wa DAWASA wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya




Waandishi wa Habari Wakimsikiliza Mkuu wa Wilaia ya Ilala

wadau mbalimbali waliohudhuria kwenye mkutano uliokuwa unajadili ombi taftishi juu ya maombi ya kurekebisha gharama za malaka ya majisafi na majitaka (Dawasa) ili kurekebisha bei za huduma ya mamlaka hiyo. Picha na Elisa Shunda



Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Raymond Mushi ameitaka Mamlaka ya Majitaka na Maji Safi Mkoani Dar es Salaam (DAWASA) kufanya kazi kasi kubwa ili kuliondoa Tatizo la ukosefu wa Maji jijini hapo.Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo.
  Bwana,Mushi ametoa Rai hiyo Mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria kwenye mkutano uliokuwa unajadili ombi taftishi juu ya maombi ya kurekebisha gharama za malaka ya majisafi na majitaka (Dawasa) ili kurekebisha bei za huduma ya mamlaka hiyo-
Ambapo licha Mamlaka hiyo kukumbana na Ukata Mkubwa Fedha wanaitajika kufanya kazi kwa bidii ili wafikie malengo ya kumaliza tatizo kubwa la Maji Mkoani Dar es Salaa.
  Kwa Mujibu wa Kaimu huyo amesema kwa sasa ni asilimia ndogo sana ya Wananchi Mkoani hapo wanaopta Maji safi na kudai Jambo hilo limechangia kuongezeka kwa Mlipuko wa magonjwa mbali mbali.
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa (DAWASA) akawataka Wakazi wa Mkoa huo kulinda miundombinu ya Maji ya Mamlaka hiyo na kuacha tabia mbovu ya kushirikiana na watendaji wasiokuwa waaminifu wa DAWASA kwa kuhujumu Mamlaka hiyo

No comments