WAZIRI MWAKYEMBE NAYE AMUIGA LOWASSA,NAYE ATUMIA MAKUNDI KUTAKA URAIS SOMA HAPA KUJUA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Herrison Mwakyembe (kushoto) na Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania (SHIMBATA), Monday Likwepa
KAMA ambayo baadhi ya makada wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), wanatumia makundi ya kijamii kujipigia debe la urais wakidai
kuombwa kugombea, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Herrison
Mwakyembe, naye ameingia kwenye mbio hizo. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Hatua
hiyo inaendelea huku makada sita wa chama hicho wakiwa bado hawajaondolewa
katika kifungo cha kudaiwa kuanza kampeni mapemba kabla ya wakati.
Miongoni mwa waliofungiwa ni Edward Lowassa ambaye chama
kimemshupalia zaidi kikimtaka azuie pia makundi yaliyokuwa yakienda kwake kwa
madai ya kumshawishi agombee urais.
Wakati hali ikiwa hivyo, Dk. Mwakyembe naye katika maadhimisho ya
fainali za mchezo wa bao jijini Dar es Salaam leo, ameonekana kupitia upenyo
ule ule wa kudai kuombwa na makundi ili agombee urais Oktoba mwaka huu.
Mchezo huo, umechezwa chini ya Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzani
(SHIMBATA) ukiwashirikisha baadhi ya wazee toka wilaya zote za mkoa wa Dar,
ambao pia waliwahi kucheza mchezo huo na hayati Julius Nyerere.
Katika fainali hiyo, Dk. Mwakyembe ndiye aliandaliwa kuwa mgeni
rasmi, akiwa mlezi msaidizi wa SHIMBATA, ambapo baada ya kukagua mchezo huo,
wazee hao wakamsomea risala ya kumpamba.
Wamesema kuwa, lengo la kumuandikia risala hilo ni kumtaka achukue
fomu ya urais.
“Sisi wazee wa mkoa wa Dar, baada ya kuwaangalia na kuwachunguza
watendaji wote wa Serikali, tumebaini kuwa Mwakyembe- mbunge wa Jimbo la Kyela,
anastahili kuwania nafasi ya urais kwa sifa alizo nazo,” wamesema.
Dk.Mwakyembe baada ya kupata maombi hayo aliwashukuru kwa mtazamo
wao na kuwaahidi kulifanyia kazi.
“Asanteni sana kwa sifa hizo, kama ni za kweli, nimezipokea,
naombeni muda wa kutafakari hilo kisha nitawapatia jibu. Ila kuhusu mchezo huu
mliouonyesha hapa nimeupenda kwani ni njia pekee ya kudumisha utamaduni wetu na
niwaahidi kuwasaidia katika hilo,” amesema Mwakyembe.
No comments
Post a Comment