RAIS KIKWETE AWAACHA WAFANYAKAZI NJIA PANDA,SOMA HAPA KUJUA

PAMOJA na wafanyakazi kumtega Rais Jakaya
Kikwete, aongoze kima cha chini cha mshahara kufikia Sh. 315,000 kwa sekta ya
umma, Sh. 220,000 kwa sekta binafsi na kupunguza kodi ya mapato toka asilimia
12 hadi tisa, majibu yake hayakutoa mwelekeo kama itawezekana. Anaandika Pendo Omary …(endelea).
Katika hotuba ya Rais kwa wafanyakazi
hao, iliyofanyika jijini Mwanza, Kikwete amesema “kiwango hicho kitaongezwa
baada ya serikali kuangalia hesabu wakati wa kuwasilisha bajeti yake ya
2016/16.”
“Tumejitahidi
kuongeza mishahara kila mwaka. Ongezeko ni dogo lakini si haba. Mwaka huu,
tutaongeza tena. Kwa upande wa sekta ya umma tutaangalia hesabu kama tutafikia
Sh. 315,000. Kama hatutafikia itakuwa ni kidogo,”amesema.
Kuhusu ongezeko
la kima cha chini cha mshahara kwa sekta binasi, Rais Kikwete amesema, Bodi za
Mishahara za kisekta ndizo zinahusika katika kushughurikia suala hilo.
“Bodi za mishahara za
kisekta zinakutana kila baada ya miaka mitatu. Mara ya mwisho kukutana ilikuwa
mwaka 2013. Mwakani zitakutana tena. Zitashughurikia suala hili,”ameeleza Rais Kikwete.
Aidha, Rais
Kikwete amesema kwamba kuhusu punguzo la kodi ya mapato inayokatwa kwenye
mapato ya wafanyakazi, serikali imekuwa ikipunguza mara kwa mara na itaendelea
kupunguza.
“Tulikuta kodi
ikiwa ni asilimia 18.5. Sasa ni asilimia 12. Mwaka huu tutaendelea kupunguza.
Sijui kama tutafikia asilimia tisa. Kama tutabakisha kufikia asilimia tisa
itakuwa ni sehemu ndogo sana,” amefafanua.
Rais Kikwete alikuwa akijibu hotuba ya Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), iliyosomwa na Katibu Mkuu wake, Nicholaus Mgaya,
akiitaka serikali ya Rais Kikwete, iongeze kima cha chini cha mishahara na
kupunguza kodi ya mapato.
Mgaya amesema
changamoto nyingine zinazowakabili wafanyakazi ni baadhi yao kukosa uhuru wa
kujiunga vyama vya wafanyakazi, Wakala wa Ajira kutotii maagizo ya serikali na
upungufu wa ajira katika halmashauri;
Nyingine ni
kutokuwepo kwa ushirikishwaji kati ya wafanyakazi na waajiri, ukosefu wa ajira,
ajira za wageni kukosa udhibiti, kutetereka kwa amani ya nchi na ukuaji wa
uchumi usiokuwa na manufaa kwa wengi.
“Ukuaji wa uchumi
haujaleta manufaa kwa wafanyakazi. Kuna mgawanyo usio na udhibiti. Wapo watu
wachache kwa kutumia nyadhifa zao ndio wananufaika na ukuaji wa
uchumi,”amefafanua Mgaya.
Kauli mbiu ya
maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Mfanyakazi jiandikishe, kura yako ina thamani
kwa maendeleo yetu.”
Chanzo ni Gazeti la Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment