TAARIFA MUHIMU KUHUSU ACT-WAZALENDO,BONYEZA HAPO KUJUA
PICHANI NI KATIBU MKUU WA ACT-WAZALENDO PICHA NA MAKTABA |
CHAMA cha
Siasa cha ACT-Wazalendo kimewaomba Wanachama wa Chama hicho,wapenzi pamoja Watanzania
wapenda mabadiliko kukichangia pesa kwa
hali na mali, ili kiweze kuanza Ziara yake ya pili mikoani ya kutoa
elimu kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika uandikisha kwenye Daftari la
wapiga kura.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama
hicho Samson Mwigamba wakati akizungumza na Mtandao huu ambapo amesema
kutokana na umuhimu wa suala Daftari la wapiga kura ni wazi chama hicho
kimepanga kuwahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi ili kutimiza jukumu lao
la msingi Kikatiba.
Mwigamba pamoja na hayo amebainisha
kuwa ili chama hicho kifanikisha ziara hiyo kinawaomba watu mbalimbali nchini
kichangia Fedha za kununua Mafuta,kukodisha Magari pamoja na Fedha za kujikimu
kwa Viongozi wa ACT-Wazalendo watakapokuwa wakitoa Elimu hiyo.
Aidha,Mwigamba alizitaja njia za kuchangia
pesa ambapo ni njia mbili ambazo ni kwa MPESA
namba 0763463740 jina ni ACT POLITICAL au kwa Tigo pesa pia ni kwa namba
0715 784670 kwa jina la (ACT –TANZANIA).
Mbali na njia hiyo za simu pia Mwigamba
amesema hata kwa njia ya Benki ya NMB wanaweza kuchagia kupitia Akaunt
NO-22610004083 Jina la ACT –Tanzania.
No comments
Post a Comment