WAZIRI MEMBE AMEJIHAKIKISHIA URAIS,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni waziri membe |
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe ametangaza nia ya kuusaka Urais kiaina ili kukwepa
rungu la chama chake cha CCM. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Membe
ametangaza nia kwa aina ya pekee, baada ya kutangaza kuwa hata kuwa Waziri
kamwe katika awamu ijayo ya Serikali ya Tanzania, baada ya kumaliza kipindi
chake cha sasa.
Kauli hiyo inamaanisha kuwa
Membe hatawania tena Ubunge katika jimbo lake la Mtama mkoani Lindi. Ili uwe
waziri lazima uwe Mbunge wa jimbo au mbunge wa kuteuliwa, kutokana na kauli
hiyo inamaana kuwa hatagiombea nafasi hizo na badala yake mpango wake wa
kuwania Urais upo pale pale.
Akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya
Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Membe amesema hatorudi katika nafasi hiyo tena
baada ya kumaliza nafasi yake baada ya kumaliza muda wake.
“Sitakuwa tena Waziri wa Mambo ya Nje, hata iweje. Sitakuwa
na mkutano tena na nyinyi kwa vyovyote vile. Hili ni Baraza langu la Mwisho
kushiriki,” amesisitiza Membe.
Hata hivyo Membe hakutaka kusema kama ameamua kwa vyovyote vile
hatakuwa waziri wa wizara hiyo, atakuwa nani?.
Wakati Membe ikitoa kauli hiyo, tayari kifungo cha miezi 12
alichopewa na CCM pamoja na makanda wengine sita wa chama hicho kwa madai ya
kuanza kampeni za urais mapema kinyume na taratibu za chama hicho kikiwa
kimemalizika.
Mbali na Membe, makada wengine sita wa CCM, waliopewa kifungo ni
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Mbunge wa Sengerema, William
Ngeleja, Stephen Wasira, January
Makamba na Edward Lowassa.
No comments
Post a Comment