SERIKALI YA TANZANIA YAMRUKA RAIS WA BURUNDI,WAZIRI MEMBE APIGILIA MSUMARI SOMA HAPA KUJUA
![]() |
Waziri wa Nchi za Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akimkaribisha Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza alipokuja Tanzania siku za nyuma |
SERIKALI ya Tanzania inayosimamia mazungumzo
ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi imesema haijui alipo Rais wa Burundi,
Pierre Nkurunzinza ambaye inasemekana serikali yake imepinduliwa. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe amewaambia waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam kuwa: “mimi sijui alipo Nkurunziza”.
Taarifa
ya mapinduzi ya serikali ya Burundi ikitangazwa jana, Rais Nkurunziza
alikuwa nchini Tanzania kuhudhuria kikao cha Marais wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) kujadili mgogoro wa Burundi. Mpaka sasa hakuna taarifa za uhakikika alipo Rais
Nkurunziza.
Baadhi ya vyombo
vya habari vya kimataifa zinasema, Nkurunziza aliondoka Tanzania kuelekea
nchini kwake, lakini alishindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege
wa Bunjumbura, kutokana na uwanja huo kufungwa.
Habari ambazo
hazijathibitishwa zinasema ndege yake ilitua nchini Uganda kujaza mafuta na
baadaye kurejea nchini Tanzania.
Akizungumzia
kuhusu hali ilivyo nchini Burundi Membe amesema Afrika hawataki tena kuona nchi
yoyote, kwa sababu zozote zile, kuchukua madaraka kwa mtutu wa bunduki, badala
yake waingia madarakani kwa demokrasia.
“Tukio la jana lililaaniwa na viongozi wote. Lakini zaidi ya hayo
baraza la mawaziri wa Afrika Mashariki lililokutana jana na juzi litakutana
tena mapema wiki ijayo, kwa ajili ya kufanya tathimini ya hali ya Burundi,”
Membe amefafanua.
Chanzo ni mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment