HABARI KUBWA LEO-LOWASSA BASI TENA,MAWAZIRI WA KIKWETE WAMMALIZA,KUTEGEMEA MIUJIZA,SOMA HAPO KUJUA

UWEZEKANO wa
Edward Lowassa kutaka kugombea Urais ndani
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) umefikia mwisho .Mtandao huu umedokezwa.Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu
umezipata kutoka ndani ya CCM zinasema mpango wa kumzuia Lowassa unasukwa kwa
Ustadi mkubwa na Waziri mmoja Mwandamizi wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete
ambapo anasema “huyu lowassa anapoteza
mda tu na tushaweka mipango kwamba Jina lake tutalikata katika hatua za awali
za kinyang’snyiro cha Urais”
Kwa mujubu wa Mtoa taarifa huyo kwa
Mtandao huu amesema Lowassa ambaye ni Waziri mkuu aliyejiuzulu
kwa Kashfa ya Ufisadi kwenye Kampuni Tata ya Richmound ambapo inaelezwa kwamba katika mkutano wa
Halmashauri kuu (NEC) na Kamati kuu uliopangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii
utakuwa na kazi ya kuliondoa jina kabla
ya muda wa kuchukua Fomu kuwadia.
Kwa mujibu wa Mipango hiyo inayosukwa na
Waziri huyo Mwandamizi umejikita kwenye Hoja ya kwamba Lowassa ameanza kampeni
mapema kabla ya chama chake akijatoa mwongozo,pili ni kujenga mtandao ndani ya
chama na kujikita kupanga safu za uongozi jambo ambalo waziri huyo anasema ni
kukidhofisha Chama hicho.
Mbali na madai hayo pia Lowassa
anatuhumiwa kuzunguka nchi nzima kufanya
Mikutano na Baadhi ya wajumbe wa (NEC ) ,wenyeviti wa Mikoa na makada
mbalimbali ngazi za kata na kuwapa pesa ili wamshawishi mwenye Mbio zake za
Urais.
Chanzo hicho kinadai Lowassa ambaye ni
Mbunge wa Munduli alikuta na wajumbe wa NEC na baadhi ya wenyekiti wa mkoa
kanda ya ziwa Viktoria pamoja viongozi wa madhehebu ya kidini kati ya mei 2013
na januari mwaka jana.
Mpango
huo wa kumkata Jina unakuja ikiwa Teyari Lowassa mwenyewe ameyakataza makundi
mbali mbali ya kijamii waliokuwa wanakwenda kumshawishi kwa kusema chama chake
kimekataza na kuwataka kusubili kwanza.
Lowassa ambaye pia ni Miongoni mwa
Makada wa Chama hicho ambao wanataka Urais Kwa udi na Uvumba ambapo kwa Mujibu
wa Wapambe wake wanasema wapo teyari kumuingiza ikulu kwa Machela ya kubeba
wagonjwa.
Taarifa hizo zinakuja ikiwa teyali
chama hicho kwa kupitia Katibu wake wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauya
kutangaza ratiba ya Vikao vya NEC na CC
vilivyopangwa kufanyika Mjini Dodoma Kuanzia 20 mei hadi 22,ambapo pamoja na
mambo mengine ni vitajadili na kuhitimisha suala la adhabu la makada wake sita
wakiongozwa na Lowassa ambao wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuanza kampeni mapema
ya kutaka Urais.
Mbali na Lowassa makada wengine waotarajiwa
kujadiliwa kwenye Kikao hicho ni Waziri mkuu wa awamu ya tatu Frederick Sumaye,
Waziri wa Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe,Waziri wa Kilimo ,chakula na
Ushirika Steven Wasira,Naibu waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia
January Makamba pamoja na Mjumbe wa NEC ambaye amesemamishwa kutokana na Ufisadi wa ESROW William Ngeleja.
Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu amesema
Mikutano hiyo mbali ya kuwajadili makada hao pia itatoa Ratiba ya na utaratibu
wa kuchua fomu za kugombea nafasi mbali mbali.
Taarifa
za Vikao hivyo zinakuja ikiwi ni wiki moja kupita baada ya Mtandao huu kufichua
mipango ambayo inapangwa ya kwenda kuvuruga vikao hivyo kabla ya kukutana na ‘kuyachinja’
majina hayo.
“Kwa sasa waziri (jina tunalihifadhi) ameshamkabidhi
majukumu yote mwenyekiti wa CCM (bara) Philip Mangula kulikata kabisa jina lake
na kuwa na hoja zinamshiko ambazo
watatumia kuliondoa jina la lowassa”amesema mtoa taarifa huyo
Sanjari na hayo pia kwa sasa Chama hicho
kikongwe barani Afrika kimepanga kubadili mfumo wake wa uchukuaji fomu na
kuweka mfumo wa mpya wa uchukuaji ambao
unawaradhimu makada wa chama hicho kutakiwa kujitangaza kupitia
vyombo vya Habari lengo ni kuwakaba
makada wake.
Mpango wa Kulikata jina la lowassa unasukwa
kwa Ustadi mkubwa na wa Ajabu na baadhi ya Mawaziri wa Rais Kikwete pamoja na
Idara ya Usalama wa Taifa ambao kwa mujibu ya wao wanasema mipango hiyo
imebarikiwa na nguvu zote ma Rais Kikwete mwenyewe.
No comments
Post a Comment