VURUGU KUBWA MSIKITINI,WAISLAM WAZICHAPA KAVU KAVU,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu msikiti mkuu wa Ijumaa Gongoni mjini Tabora, uliwahi kukumbwa na vurugu siku za nyuma |
WATU wawili waumini wa
dini ya Kiislamu, wamejeruhiwa katika vurugu zilizoibuka kwenye Msikiti wa
Hidayah kata ya Kitangiri jijini Mwanza. Anaandika Mwandishi
Wetu … (endelea).
Kufuatia vurugu hizo, Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mwanza, limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waumini hao
huku wawili wakitiwa mbaroni.
Vurugu
hizo zilianza saa moja usiku wa kuamkia Mei 15 mwaka huu, kufuatia kijana mmoja
kujitokeza mbele ya Msikiti huo akitaka kusoma barua ilidaiwa kuchochea fujo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna
Mwandamizi Msaidizi, Charles Mkumbo, amesema vurugu hizo zilizuka jioni wakati
waumini hao wakiswali, ndipo ghafla alitokea kijana mmoja ambaye hakufahamika akitaka
kusoma barua.
Mkumbo amesema baada ya waumini hao
kumkataza kusoma barua hiyo, lilitokea kundi la vijana wengine na kuingia
kwenye Msikiti huo wakiwa na mapanga na marungu na kuanza kufanya fujo katika
msikiti huo.
“Baada ya kuona vurugu hizo zinaendelea,
tulilazimika kutumia nguvu ya ziada kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya na
kufanikiwa kutuliza ghasia hizo. Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani
pindi upelelzi utakapokamilika,” amesema Mkumbo.
Mmoja wa waumini, Kawawa Kiumba,
ameliambia Chanzo changu kuwa, kufuatia mapigano hayo, Serikali inapaswa
kuingilia kati kumaliza mgogoro uliopo kati ya Haswali Suna na Suni Jamaa
wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani.
Amesema serikali
inapaswa kuingilia kati mgogoro huo kutokana na kuwepo baadhi ya watu wachache
wanaotumia mwanya huo kujinufaisha wao wenyewe badala ya kumwabudu Mwenyezi
Mungu.
“Mimi nadhani hao
vijana waliofanya fujo walikodishwa ili kuonekana kuna mgogoro, na hiyo yote
kuna matajiri wachache ambao wameshindwa kuwaunganisha waumini hawa na badala
yake wanakuwa chachu ya fujo,” amesema Kiumba.
Mwenyekiti wa Mtaa wa
Medical Research, Patroba Maginga, amesema kitendo cha vurugu hizo
kinasababisha wananchi kuathirika na kuacha kufanya shughuli za kimaendeleo
ambazo zinawaingizia kipato.
Hata hivyo, amesema
vurugu hizo haziwaathiri waumini pekee bali na wananchi wengine, hivyo ni vyema
serikali ikaingilia kati ili kutafuta muafaka wa jambo hilo kabla tukio halijajirudia.
Chanzo ni Mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment