KAMANDA KOVA AZIDI WEKA HISTORIA JIJINI DAR-AZINDUA HUDUMA BORA YA DHARULA SOMA HAPO KUJUA

WAZIRI wa Mambo ya
Ndani, Mathias Chikawe, amezindua rasmi mradi wa simu za dharura kwa Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Namba hizo ni 111 na 112. Anaandika
Sarafina Lidwino … (endelea).
Uzinduzi
huo umefanyika katika uwanja wa makao makuu ya kanda hiyo, ambapo viongozi
mbalimbali walihudhuria akiwemo Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia,
Prof. Makeme Mbarawa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Dk. Joseph Kilongola na Makamishna Suleiman Kova.
Akiuzungumzia mradi huo, Kilongola kwa
niaba ya TCRA amesema, lengo la kuazisha mawasiliano hayo ya dharura lilianza
tangu mwaka 2013 ambapo walishirikiana na Jeshi la Polisi hadi kufikia leo.
Amesema, waliamua kufanya hivyo baada ya
kutokuwa na kituo cha simu za dharura Polisi kwa muda mrefu kutokana na
uharibifu wa miundombinu ambapo mvua iliharibu mitambo ya mawasiliano.
“Baada ya shida hiyo ya muda mrefu,
ndipo TCRA ikatoa tena kiasi cha Sh. 50 milioni kwa ajili ya kurudisha mitambo
iliyoharibika, kukarabati chumba cha kuweka mitambo hiyo, pamoja na kutoa
mafunzo kwa maafisa 65 watakaotoa huduma hizo,” amesema Kilongola.
Naye Kova, amesema,
“…tunawashukuru sana TCRA kwa kudhamini mradi huu, kwani wananchi
wamepata tabu kwa muda mrefu jinsi ya kutoa taarifa za uharifu. Tunaimani
kuwepo kwa namba hizi kutapunguza uharifu nchini.”
Aidha, Kova amesema,
kuna kompyuta 12 za kupokea simu kwa wakati mmoja na zina uwezo wa kurekodi na
kuhifadhi taarifa zote za mpigaji simu, pia mitambo ina uwezo wa kupokea simu
kutoka mikoa yote.
Kwa upande wake,
Chikawe amewasihi wananchi kuitumia fursa hiyo kwa kutoa taarifa muhimu na sio
kufanya mizaha.
“Pia nitoe rai kwa
maafisa wote mliofundishwa kutumia mitambo hiyo kuwa wasikivu na kuyapokea
matatizo ya wananchi. Isije kutokea mtu ana dharura anapiga simu bila kupata
msaada, pia msiwe wakali kwa wapigaji simu,” amesema Chikawe
Chanzo ni Mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment