MORSI AHUKUMIWA KUNYOGWA MPAKA KUFA SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Aliyekuwa Rais wa Misri, Mohamed Morsi akiwa gerezani alipohukumiwa kifungo cha miaka 20 |
ALIYEKUWA Rais wa Misri, Mohammed Morsi amehukumiwa kunyongwa
mpaka kufa na Mahakama moja nchini Misri baada ya kukutwa na hatia.
Kwa
mujibu wa mtandao wa BBC, Mahakama hiyo ilimpata na hatia Morsi kufuatia
kuvunjwa kwa magereza mwaka wa 2011.
Kauli hii ni msumari katika kidonda cha
Morsi ambaye alikuwa tayari anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kuamrisha
kukamatwa kwa waandamanaji waliopinga utawala wake.
Morsi aling’olewa madarakani na jeshi
Julai, 2013 kufuatia kipindi kirefu cha maandamano dhidi ya utawala wake.
Kuanzia hapo chama chake cha The
Muslim Brotherhood kimepigwa marufuku huku mamia ya maelfu ya wafuasi wake
kukamatwa na vyombo vya dola.
Kufuatia uamuzi huo wa kifo,
sasa kauli nzima na ruhusa itapatikana tu baada ya uamuzi kutumwa kwa kadhi
mkuu nchini humo ambaye sasa ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho iwapo Morsi
ataonja mauti au la.
Sheria za nchi hiyo hata hivyo
zinamruhusu Morsi kukata rufaa licha ya uamuzi wa kadhi mkuu.
Morsi aliweka rekodi ya kuwa
kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru.
Hata hivyo utawala wake
ulikumbwa na wimbi la maandamano baada ya kujilimbikizia madaraka akiwa
amehudumu kwa mwaka mmoja tu ya kuwa ofisini.
No comments
Post a Comment