SERIKALI YAJITWISHA GUNIA LA MISUMARI BVR,WAZIRI MHAGAMA AMJIBU MBOWE NA LIPUMBA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge), Jenister Mhagama |
PAMOJA na kazi ya
uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu kwa mfumo wa kielektroniki
(BVR) kuambatana na kasoro lukuki, Serikali imeahidi kuwa kazi hiyo itakamilika
ndani ya siku 60.Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Jenista Mhagama-Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge), ndiye ametoa ahadi hiyo bungeni mjini
Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia hotuba ya Bajeti kwa ofisi
ya waziri mkuu 2015/16.
Amesema “ndani ya siku 60 (miezi miwili),
kazi hiyo itakuwa imekamilika kutokana na kuongezwa kwa mashine za BVR. Kwa
sasa zipo BVR kits 4,850 na serikali inategemea kupokea zingine 3,150 ili
kufikisha jumla 8,000.”
Kwa mujibu wa Mhagama, baadhi ya mikoa
kama Njombe, uandikishaji tayari umekamilika.
Ameongeza kuwa, kutoka
na kuwepo kwa idadi hiyo ya mashine, kuna uwezekano wa kuandikisha watu 800,000
kwa siku iwapo kila mashine moja itaweza kuandikisha watu 100.
“Iwapo mashine hizo zikitumiaka
kuandikisha watu 100 kwa siku, hivyo ni wazi kuwa ndani ya siku 60 kazi ya
uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura litakuwa limekamilika.
Ametaja mikoa mingine ambayo inatarajiwa
kuanza kuandikishwa Mei 18 mwaka huu, kuwa ni Dodoma, Singida, Mbeya, Rukwa,
Kigoma, Kagera, Katavi na Tabora.
Amesema kuwa kwa sasa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi inaendelea na uandikishaji katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Kuhusu mshauri juu ya uboreshaji wa
daftari la wapiga kura na kutumia mashine za BVR, Mhagama amesema kuwa,
walikataa ushauri huo kutokana na kubaini kuwa ilikuwa ni gharama kubwa zaidi.
Amefafanua kuwa, jinsi mshauri huyo
kutoka Marekani alivyowashauri, ilionekana kuwa gharama ingekuwa zadi ya Sh.
321 bilioni badala ya Sh. 293 za sasa.
“Ikumbukwe kuwa uboreshaji daftari
mwaka jana, uligharimu Sh. 72 bilioni na kama matumizi ya mashine ni Sh. 218
bilioni, jumla zingekuwa Sh. 321 bilioni,”amesema.
Akizungumzia uchaguzi wa Zanzibar,
Mhagama amesema “masuala ya uchaguzi yatasimamiwa na Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar (ZEC). Hata hivyo, uhakika ni kwamba daftari litaboreshwa zaidi.”
Kwa mujibu wa Mhagama, wapinzani
wamekuwa wakilalamikia juu uboreshwaji wa daftari ya kudumu la wapiga kura na
kuhofia uchaguzi mkuu ujao kutofanyika.
Chanzo ni
mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment