HABARI KUBWA LEO-LOWASSA APATA JANGA TENA,KAMATI YAKE YAVURUGIKA,AMUANGUKIA BILIONEA ROSTAM AZIZI,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Pichani ni Edward lowassa |
KILE
kinachoonekana ni kwamba Mambo yameanza kuwa magumu ndani ya Kambi ya Edward
Lowassa katika harakati zake za kuwania Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM ,Baada
ya Kambi yake kuanza kubomoka,Mtandao huu umebani.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu
umezipata zinasema mwenyekiti wa Kamati
ya wezesha Lowassa aingie ikulu Bwana Colnel Apson Mwang’onda amejitoa kwenye Nafasi hiyo.
Ambapo kwa Mujibu wa Vyanzo hivyo
zinasema Mwang’onda ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa mstaafu
inasemekana sababu ya kutimka kwenye Nafasi hiyo inatajwa ni Kuwa na mahusiano
mabaya ya hivi karibuni na Edward Lowassa.
Mwang’onda ambaye aliteuliwa kwenye
Nafasi hiyo na Lowassa mwezi Mei mwaka juzi akipewa jukumu la kuhakikisha
anamsafisha Kada huyo wa CCM anayeutaka Urais kwa udi na Uvumba kwenye Kashfa
mbali mbali ambazo zinatajwa kuhusika kwake.
Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu aliyoko
kwenye Kamati ya wezesha lowassa aingie Ikulu zinadai kwa sasa Lowassa ameanza
kumuangukia Aliyekuwa Mbunge wa Igunga Mashariki na Mfanyabiashara maarufu
nchini bwana Rostam Azizi ili achukue nafasi hiyo ya Mwang’onda.
Rostam Azizi ambaye alijuzulu nafasi ya
Ubunge pamoja na Nafasi mbalimbali za Chama cha mapinduzi CCM,akidai kwamba “kuna siasa Uchwala ndani ya CCM”
Mbali na Kujiuzulu huko
Mfanyabiashara huyo pia alikuwa miongoni mwa watu waliounda magenge mbalimbali
yalihusika kuhakisha Rais Jakaya Kikwete
anaingia Ikulu mwaka 2005 ikiwemo kutoa fedha zake banasfi.
Ambapo Duru za kisiasa zinasema kuondoka
huko kwa Mwang’onda kumeiacha pengo kubwa sana kwenye kambi ya Waziri mkuu huyo
aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi kwenye
Kampuni Tata ya Richmound.
“Sikufuchi
kitendo cha kuondoka bwana huyo ni wazi kambi ya Lowassa itakosa nguvu kabisa
,kwasababu huyu mtu anajua siri nyingi za lowassa unategemea kuondoka huko
kunaweza kumweka pabaya Lowassa”
“Halafu kingine hawa usalama wa Taifa
hawaaminika sana maana ni watu hatari sana,tena sio wa kuwaamini kabisa
nashangaa sana lowassa alimpa nafasi kubwa kiasi hicho,na huyu lazima atakwenda
kupeleka nguvu kwenye Kambi zengine tofauti na lazima utaona”
No comments
Post a Comment